26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

GCLA yakaribisha wadau kuboresha haki jinai

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imewahimiza Watanzania kuitumia ili kuboresha mfumo wa haki jinai nchini na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji haki kwa wakati.

Mamlaka hiyo inatumia Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuelimisha umma kuhusu shughuli mbalimbali inazozifanya zikiwemo za kurugenzi ya huduma ya sayansi jinai.

Akizungumza Januari 27,2024 katika maonesho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Sayansi Jinai, Fidelis Segumba, amesema masuala ya haki jinai yanahusisha kufanya uchunguzi wa kimaabara wa sampuli ama vielelezo mbalimbali ambavyo vinahusiana na matukio ya jinai.

Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Sayansi Jinai, Fidelis Segumba, akimsikikiza mteja katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

“Ni maabara yetu Watanzania hivyo vyombo vyote vitumie maabara hii kwa ajili ya kuweka haki jinai katika kiwango cha kisasa zaidi.

“Uchunguzi wote unaofanywa upande wa sayansi jinai mwisho wake huwa ni kutolea ushahidi mahakamani kufafanua matokeo yaliyopatikana maabara.

“Tunatumia maonesho haya kuelimisha wadau mbalimbali, taasisi za Serikali na wananchi kupata ufahamu ili tuzidi kuboresha haki jinai katika jamii yetu,” amesema.

Amesema kuna maabara ya vinasaba vya binadamu ambayo inahusika kuchunguza matukio mbalimbali kama ya ubakaji, mauaji, kujeruhiwa na mengine ambapo uchunguzi hufanyika ili kutambua wahusika.

Maabara nyingine ni ya uchunguzi wa kutambua sumu inayotumika kumdhuru au kumuua mtu ili kuokoa maisha ya mtu aliyedhurika au kuweka ushahidi zaidi wa sumu iliyotumika.

“Tunayo maabara ya sayansi kemia ambapo hutambua dawa za kulevya, aina, ujazo kubaini aina za kemikali zilizotumika kuchochea milipuko au moto sehemu mbalimbali,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles