27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko asisitiza weledi Mamlaka za ununuzi wa Umma Afrika Mashariki

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki, kuzingatia weledi, maadili na uwajibikaji ili kuleta ufanisi uliokusudiwa.

Dk. Biteko ametoa agizo hilo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma kwa nchi za Afrika Mashariki na uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) lililofanyika leo Septemba 9, 2024 jijini Arusha.

Amesema Serikali zinatambua kwamba fedha nyingi zinazotengwa kwenye bajeti kila mwaka zimekuwa zikitumika kupitia ununuzi wa umma, kwa kuzingatia hilo, Serikali imekuwa makini kuhakikisha kuwa fedha hizo kupitia ununuzi wa umma zinapata usimamizi makini.

“ Naomba Waziri wa Fedha mlisimamie hili na haya ni maelekezo ya Mhe. Rais kupitia majukwaa yaliyofanyika yote yametilia mkazo maadili, weledi, uwazi na uwajibikaji na bila maadili wananchi hawezi kupata huduma.

“Pia fedha nyingi zinazotengwa kwa ajili ya wananchi kupata huduma zinaamriwa na kundi hili na kama hatuna taasisi imara za ugavi na ununuzi hatutapata matokeo ya fedha na hatimaye umasikini utaongezeka,” amesema.

Ameongeza kuwa “Nawaomba mnapojadili leo mkumbushane umuhimu mkubwa wa kulinda taaluma yenu, ioneeni wivu isimamieni taaluma yenu akitokea mtu anafanya vitendo visivyofaa mkemeeni. Jisimamieni wenyewe, asitokee mtu katikakati ya manunuzi anataka kufanya vitendo visivyofaa, PPRA simamieni vizuri jambo hili ili kuhakikisha thamani ya fedha inapatikana,”

Aidha Dk. Biteko amewapongeza washiriki kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushiriki jukwaa hilo ambao kupitia jukwaa hilo watapata fursa ya kubadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kujadili masuala muhimu yanayohusiana na ununuzi wa umma kwenye nchi za Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba amesema kuwa majukwaa hayo hukutana kupitia nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo huwa na majadiliano na maazimio na katika Jukwaa la 16 washiriki watapata fursa ya kuangalia utekelezaji wa maazimio ya jukwaa la 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles