28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yaja na kampeni ya ‘Vuna Point -Endesha Boda’

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Katika kuadhimisha miaka tisa ya Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, imezindua huduma mpya iliyopewa jina la ” Vuna Point -Endesha Boda”, kampeni hiyo ikiwalenga wateja wake waliopo mjini na vijijini.

Akizungumza na waandhishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 10,2024, Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio, amesema katika kampeni hiyo wateja wana nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwamo pikipiki ‘boda boda’ mpya kila mwezi.

“Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi kwani wateja wetu wanatakiwa kujikusanyia point kwa kuweka vocha ya kukwangua au kufanya miamala ya Halopesa ambapo utaweza kuvuna pointi kisha kununua namba ya bahati kupitia 14866# au kwa kutumia App ya Halopesa kisha ‘9’. amesema Kadio.

Kwa Upande wake Naibu Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja, Shaban Said, amesema kuwa sherehe ya miaka tisa ya huduma ya Halotel na kampeni hiyo,ni mafanikio ambayo hayawezi kutenganishwa na imani, uamimifu wa wateja wetu na hiyo ni moja ya shukrani kwao.

“Kampeni tuliyoizindua leo ni shukrani kwa wateja walioenda nasi ndani ya miaka tisa ya huduma yetu hivyo nawaomba Watanzania watumie kampuni yetu ya mawasiliano ili waweze kutimiza malengo yao ya mawasiliano mjini na vijini,” amesema Shaban.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles