23.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 2, 2024

Contact us: [email protected]

DC Machali azindua jengo la Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Mkalama

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali leo amezindua jengo la Dawati la Jinsia na Watoto linalopatikina katika kituo kikuu cha polisi wilayani Mkalama ikiwa ni jihudi ya serikali katika kutokomeza ukatili wa kijinsia nchini Tanzania

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo Juni 29,2024 amewataka wakazi wilayani Mkalama kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani Mkalama

“Kila mmoja ahakikishe anapambana kutoa taarifa kuhusu ukatili wa kijinsia kwenye mamlaka zinazohusika, tutumie Jeshi letu la polisi vizuri. Sisi sote tunapaswa kuwa mashujaa katika mapambano haya,” Machali.

Aidha Mhe. Moses Machali amewasisitiza wazazi Wilayani Mkalama kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kutimiza ndoto zao za kimaisha na mzazi atakayekataa kumpeleka mtoto shule serikali itamchukulia hatua kali dhidi yake.

Kwa Mujibu wa taarifa ya Kamishina wa Kamisheni ya Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile, amesema vitendo vya ukatili vimeongezeka nchini kwa mwaka 2023 kulinganisha na mwaka 2022 huku moja ya sababu ya kuongezeka kwa vitendo hivyo ni kutokana na uelewa mkubwa wa jamii katika kuripoti matukio ya ukatili kulinganisha na miaka ya nyuma.

“Kwa mwaka 2023 vitendo vya ukatili viongozeka hadi kufikia 22,147 kulinganisha na matukio 18,403 kwa mwaka 2022 kwa watu wazima na kwa upande wa watoto matukio yaliyoriptiwa ni 15,301 kulinganisha na 12,162 kwa mwaka 2022 “CP Faustine Shilogile

Naye Naibu Mwakilishi Mkazi UNWOMEN Ms Katherine Gifford amelipongeza Jeshi la Polisi nchini Tanzania na serikali kwa ujumla kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles