ILI kuepuka mimba zisizotarajiwa, wanawake wengi huamua kutumia vidonge vya kuzuia ujauzito (vidonge vya uzazi wa mpango/majira). Vidonge hivi huwa na madhara mengine mabaya hapo baadaye vikitumika kwa kipindi kirefu.
Zipo dawa za asili kadhaa nyingi zaidi ya 20 ambazo zinaweza kutumika kama njia za kuzuia ujauzito usiotarajiwa bila kukuachia madhara yoyote mabaya. Dawa hizi ama zinazuia urutubishaji wa yai moja kwa moja au huweza kukusababishia kuona siku zako na hivyo kuondoa uwezekano wa kuwa mjamzito.
Leo nitakujulisha dawa asili ambazo husaidia kuzuia ujauzito.
Jambo la kuzingatia ni kwamba kama itatokea umepima na kugundulika ni mjamzito basi usizitumie kwani inaweza huharibu (miscarriage).
Dawa za uzazi wa mpango kwa wanaume
1. Papai
Mbegu za papai ni dawa nzuri ya uzazi wa mpango kwa upande wa wanaume. Zinapunguza idadi ya wingi wa mbegu za mwanamume (sperm count) na zinaweza kushuka mpaka kufika sifuri (zero sperm count) na hivyo mwanamume hukosa uwezo wa kutungisha mimba. Ukihitaji kuzaa tena unaacha tu kuzitumia na hali yako itarudi kama kawaida. Kula mbegu za papai kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara moja kila siku.
Unaweza kuanza zoezi hili wiki tatu kabla hujaamua rasmi kama ndiyo dawa yako ya uzazi wa mpango.
Watu wa Bara la Asia wamekuwa wakitumia mbinu hii tangu miaka mingi iliyopita na haina madhara yoyote.
Dawa za uzazi wa mpango kwa wanawake
2. Mbegu za nyonyo
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Kano State College of Arts, Science and Remedial Studies cha Nigeria, wamethibitisha kuwa mbegu za nyonyo zinaweza kutumika kama dawa ya uzazi wa mpango. Mbegu hizi hutumika kwa miaka mingi nchini India kama dawa ya uzazi wa mpango.
Unachotakiwa kufanya ni kunywa na maji mbegu nne mpaka tano kwa siku kila siku wakati wa siku zako na zitakupa kinga karibu kwa mwaka mzima. Menya ganda lake la nje kabla ya kumeza.
Siku mbili au tatu za mwanzo za kutumia unaweza usijisikie vizuri, kupata pumzi fupi, vipele (rashes), kizunguzungu, kutapika au kuharisha. Lakini baadaye hali hiyo hutulia.
3. Tangawizi
Tangawizi huhamasisha kutokea kwa siku zako. Kunywa vikombe vitatu mpaka vinne vya chai ya tangawizi kila siku ili kuzuia ujauzito. Chota kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa tangawizi na uweke ndani ya maji ya moto kikombe kimoja (robo lita/ml 250) na unywe yote (unaweza kuongeza asali kidogo kupata ladha). Fanya zoezi hili kutwa mara tatu mpaka mara nne kwa siku tano tangu ufanye tendo la ndoa bila kinga. Unaweza pia kutumia tangawizi mbichi kwa matokeo mazuri zaidi.
4. Kotimiri (Parsley)
Kotimiri inapatikana kirahisi jijini Dar es Salaam na Visiwani Zanzibar na ni kiungo muhimu kwenye mahoteli nyingi za kitalii. Kunywa kikombe kimoja (robo lita/ml 250) asubuhi na jioni cha chai iliyoandaliwa, ukitumia kotimiri mbichi kila siku ili kuzuia ujauzito usiotarajiwa. Hakuna madhara yoyote mabaya ya matumizi ya dawa hii.
5. Vitamin C
Vitamini C ikitumika katika hali yake ya uasili kabisa inaweza kutumika kama dawa ya uzazi wa mpango. Kwenye vitamini C kuna ‘ascorbic acid’ ambayo huzuia homoni inayouandaa mji wa uzazi (‘progesterone hormone’) kushindwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo mimba kukosa mahali pa kukaa baada ya yai kurutubishwa.
Meza viponge vya vitamin C mg 1500 mara mbili kwa siku mbili mpaka tatu baada kushiriki tendo la ndoa bila kinga. Vitamin C ni nzuri pia kwa ngozi yako.
Mambo ya kuzingatia
1) Usitumie kiasi kingi cha vitamini C kwani inaweza kuufanya mwili wako kutokuwa sawa au unaweza usijisikie vizuri.
2) Usitumie vitamini C kama unatumia dawa za kuzuia damu kuganda (anti-coagulant medications).
3) Usitumie vitamini C kama una tatizo la sickle cell (selimundu).
Kumbuka kuwa makini mara zote na wewe fanya utafiti binafsi pia.
Mwandishi wa makala haya ni Fadhili Paulo amabye ni Tabibu wa Tiba Asilia. Kwa mawasiliano zaidi: WhatsApp +255769142586.