33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

BWANA VITA WA ZAMANI ARUDI NYUMBANI DRC

KINSHASA, DRC


KIONGOZI wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean Pierre Bemba amerudi nyumbani jana, baada ya kukaa takribani muongo mmoja kifungoni nje ya nchi.

Bemba aliyefutiwa mashataka hivi karibuni na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ameonyesha wazi nia yake ya kugombea urais nchini hapa.

Alishindwa katika uchaguzi wa urais mwaka 2006 dhidi ya Rais wa sasa, Joseph Kabila ambaye muda wake umeisha tangu mwaka 2016, jambo ambalo bado linaleta maswali mengi iwapo atagombea tena.

Kurudi kwa Bemba kunaonekana kusisimua upya na kutikisa siasa za DRC, na chama tawala tayari kimetoa tamko kuwa kiongozi huyo hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais kwa vile alikuwa mshitakiwa wa makosa ya jinai.

Vyama vimebakiwa na wiki moja ya kuwasilisha majina ya wagombea wao, na tayari chama cha Bemba kimeshamchagua kuwa mgombea wake, huku mwenyewe akisema atamuunga mkono mgombea yeyote kutoka upinzani.

Kwa upande wa Kabila, bado hajazungumza chochote juu ya kurudi kwa Bemba.

Makamu huyo wa Rais wa zamani alikuwa Ulaya kwa miaka 12, huku miaka 10 akitumikia kifungo kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na wafuasi wake katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles