30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Blaise Matuidi, Rugani wapona Corona

 TURIN, ITALIA 

NYOTA wa timu ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus, Daniele Rugani na Blaise Matuidi wametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamepona virusi vya corona. 

Uongozi wa timu hiyo umethibitisha kuwa hali ya wachezaji hao ipo sawa kwa sasa baada ya kufanyiwa vipimo huku awali wakikimbizwa hospitalini walipogundulika kuwa na virusi hivyo hatari. 

Matuidi ambaye ni raia wa nchini Ufaransa anayekipiga katika safu ya kiungo aligundulika kuwa na virusi hivyo Machi 18, ikiwa ni wiki moja baada ya beki wa timu yao ya Juventus, Rugani kugundulika. 

Mabingwa hao wamedai kwa sasa wachezaji hao wapo sawa baada ya kufanyiwa vipimo vipya na kuonekana hawana virusi vya corona, hivyo kwa sasa wachezaji hao wanatakiwa kukaa kwa kujitenga na familia zao kwa muda. 

“Rugani na Matuidi wamefanyiwa vipimo vipya baada ya hali yao kuonekana kuwa sawa, hivyo vipimo hivyo vimeonekana kuwa vizuri wawili hao hawana tatizo tena la virusi vya corona. Wametakiwa kurudi nyumbani.” Waliandika Juventus. 

Hata hivyo Matuidi amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa, bado ataendelea kuwa mchezaji wa timu hiyo kwa muda mrefu huku akiwa amesaini mkataba ambao utamfanya hawe hapo hadi 2021, mkataba huo aliusaini Februari 14, kabla ya mkataba huo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 alitarajia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu. 

Kwa upande wa Rugani yeye aliwashukuru mashabiki kwa maombi yao na kuwafanya wachezaji hao kurudi katika hali zao za kawaida. 

“Mashabiki zangu mko tayari kusikiliza habari njema kutoka kwangu, najua wapo ambao walikuwa na wasiwasi na mimi kutokana na hali yangu baada ya kukutwa na virusi vya corona, lakini niwaambie kuwa kila kitu kipo sawa sasa na sina tena virusi hivyo,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles