24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

RIHANNA, JAY-Z waingia tena mifukoni

 NEW YORK, MAREKANI 

NYOTA wa muziki ambaye pia ni mfanya biashara, Rihanna Fenty na rapa Jay Z, wameungana pamoja na Mkurugenzi wa Twitter, Jack Dorsey na kukusanya kiasi cha dola milioni 6.2, ambazo ni zaidi ya bilioni 138 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia kupambana na virusi vya corona. 

Rihanna kupitia Clara Lionel Foundation, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 32, amesema fadha hizo zitakwenda kuungana na zile za mashirika mengine kupambana na kuenea kwa virusi hivyo. 

Wakati huo fedha Jack na Jay-Z kupitia Shawn Carter Foundation, fedha zao zinakwenda kutumika kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali United States, Caribbean pamoja na nchi za Afrika katika jangwa la Sahara. 

Wiki moja iliopita Jay Z na Rihanna waliungana pamoja na kila mmoja aliingia mfukoni na kutoa kiasi cha dola milioni mbili na kukusanya dola milioni nne kwa ajili ya kusaidia kupambana na virusi hivyo. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles