32.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: Puuzeni uzushi hakuna vanila inayouzwa milioni 1 kwa kilo

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa rai kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kufuatilia bei ya mazao katika mitandao mbalimbali ya kimataifa ili kuepuka uzushi unaoweza kujitokeza kwenye baadhi ya bei za mazao.

Hayo ameyasema September 3, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wahariri ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus Ikulu wenye lengo la kujadili kuhusu mkutano mkubwa wa mifumo ya chakula Afrika AGRF unaotarajiwa kufanyika Septemba 5 hadi 8, mwaka huu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

Amesema Watanzania wengi walikuwa wakiaminishwa kuhusu kilimo cha vanila kwamba kilo moja inaweza kuuzwa kwa Sh million 1 hadi 1.5 jambo ambalo siyo kweli.

“Watanzania wanapaswa kupuuza taarifa hizo ambazo zimekuwa zikitangazwa katika mitandao mbalimbali siyo kweli hiyo bei haipo hata kama ni kweli nchi ilikuwa na uhitaji wa zao hilo,” amesema Bashe.

Ameongeza kuwa Serikali hivi karibuni itatoa muongozo kuhusu zao hilo ambalo kwasasa linalimwa katika mikoa mbalimbali ikiwa ikiwamo Kagera na Kilimanjaro.

Amesema ni kweli Tanzania ilikuwa na uhitaji wa zao hilo na kwamba hiyo ni kutokana na nchi ambazo zinaongoza kwa kulima zao hilo kukumbwa na majanga mbalimbali.

“Ni kweli tulikuwa na uhitaji wa zao hilo kutokana na nchi kama Madagascar ambao ndiyo wakulima wakuu wa zao hilo ilikumbwa na kimbunga lakini siyo chanzo cha kufikia bei ya Sh milioni moja kwa kilo huo ni udanganyifu, Watanzania waupuuze wasubiri Serikali itatoa muongozo kuhusu zao hilo,” amesema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles