Na Safina Sarwatt, Mwanga
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro limeiomba serikali kudhibiti makundi ya tembo katika kata Toloha na kwako ambayo yamekuwa yakivamia mazao ya wakulima na kwamba wamekuwa tisho kwa wananchi.
Aidha, tembo hao wanadaiwa kutoka hifadhi ya Tsavo nchini Kenya.
Hayo yamesemwa February 15, mwaka huu na Diwani wa Kata ya Toloha, Palesio Makange, kwenye mkutano wa baraza hiyo halmashauri uliokaa kwa ajili ya kujadili taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Maendeleo katika Kata kwa kipindi cha Robo ya Pili Oktoba hadi Desemba 2020/2021 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwanga.
Makange amesema tembo hao wamekuwa wakivamia mashamba ya wakuli na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazoa ya wananchi nakuombe serikali kuwa fudia wananchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la madiwani wilaya ya Manga, Saleh Mkwizu amesema sula la wanyama pori halmashauri inashirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mamalaka za wanyama pori ili kuona uwezekano wa kuwadhibiti wanyama hao.