TADA Cup kuunguruma Machi 26

0
263

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Mashindano ya Kombe la TADA(TADA Cup) yamepangwa kufanyika Machi 26 hadi 28, mwaka huu jijini Dodoma.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz, Makamu Mwenyekiti wa TADA, Redmpta Mwabesa, amesema lengo ni kupata Mabingwa wa mchezo huo.

Amesema mashindano hayo yatashirikisha mchezaji mmoja mmoja, wawili wawili na timu.

“Tunaomba wachezaji kutoka mikoa mbalimbali wajipange vyema kuhakikisha wanonyesha ushindani mkubwa mwaka huu,” amesema Redmpta.

Makamu huyo amewata viongozi wa mikoa yote kuhakikisha wanawaandaa wachezaji wao wanakuwa tayari kwa mashindano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here