33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru Dodoma yarejesha fedha na nyumba zilizotaifishwa na kampuni ya Geneva Credit Shop

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kuzirejesha zaidi ya Sh milioni  176,000 na nyumba moja kwa watu 17 ambao walikopeshwa na Kampuni ya Geneva Credit Shop ya Wilayani Kondoa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 18, mwaka huu, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sostenes Kibwengo, amesema mwezi uliopita Takukuru ilieleza wanafanya uchunguzi dhidi ya Kampuni ya  Geneva Credt Shop ya Wilayani Kondoa inayojishughulisha na ukopeshaji wa fedha mara baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka wananchi.

Kibwengo amesema uchunguzi wa Takukuru mkoani humo umefanikiwa kumpata mmiliki wa kampuni hiyo, Abubakary Kinyuma maarufu kama ‘Abubakari Mapesa’ ambaye hadi sasa amerejesha jumla ya Sh milioni 179,565,000 na nyumba moja.

“Leo tunawakabidhi wakopeshwaji 17 hizi fedha pamoja na hati ya nyumba hiyo,uchunguzi wetu umeonesha kwamba walilipishwa fedha hizo  na kunyang’anywa nyumba na ndugu Mapesa  kinyume na utaratibu,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles