FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Mchezo wa Bao Nchini (SHIMBATA), kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi (CCM), limeandaa tamasha la mchezo huo kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 20 ya kumuenzi hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais wa Shirikisho hilo, Monday Likwepa amesema lengo la tamasha hilo ni kumuenzi baba wa taifa kutokana na ushiriki wake katika kuinua mchezo huo kipindi cha uhai wake.
Likwepa amesema kikao cha kwanza cha maandalizi ya tamasha hilo kitafanyika Machi 27 mwaka huu katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
“Tamasha hilo litafanyika mnamo Octoba 14 mwaka huu na litashirikisha watu mashuhuri wakiwemo wanamuziki waliowahi kutunga na kuimba nyimbo za kuunga mkono harakati za Mwalimu Nyerere katika vita vya ukombozi wa Afrika, ujenzi wa taifa na kuwaletea maendeleo wananchi,” ameeleza Likwepa.