33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Matajiri kuchukuliwa hatua

HARARE, Zimbabwe

MAMALAKA nchini Zimbambwe, imesema watu ambao hawawezi kuelezea utajiri wao ulitoka wapi mali zao ziko katika hatari ya kuchukuliwa hata ikiwa mahakama itawaondolea madai ya kuhusika na ufisadi.

Mwenyekiti wa Tume ya Kupambana na Ufisadi Zimbambwe, Jaji Loyce Matanda-Moyo, alisema oparesheni mpya nchini humo ni kuchunguza maisha ya matajiri.

Nchi hiyo, inakabiliana na mdodoro wa kiuchumi katika kiindi cha mwongo mmoja sasa.

Raia wamekuwa na hasira juu ya huduma mbovu zinazotolewa, huku ufisadi ukiendelea kukithiri.

“Huu ni uchunguzi wa maisha ya baadhi ya watu matajiri. Watahitajika kutoa stakabadhi zao kuonesha bidhaa na huduma wanazatoa na zitahitajika kwendana na thamani ya mali walionao. Pia tutaangalia ikiwa watu hawa au biashara zao walikuwa wanalipa ushuru,”alisema.

Katika oparesheni hiyo, tume  inatumia madaraka iliyopata kuanzia Julai mwaka jana  ya kutaka kuelezewa jinsi watu walivyopata utajiri wao kulingana na kile kinachofahamika kama utajiri usioweza kuelezeka.

Watu wanaochuguzwa wanaweza kwenda mahakama ya juu kuelezea utajiri wao, iwapo hawatafanya hivyo moja kwa moja mali zao zinachukuliwa.

Zimbambwe sio nchi ya kwanza kuchukua hatua kama hiyo kutaka watu kuelezea vile walivyopata utajiri wao. Ireland na Uingereza zote zilibadilisha sheria zao na kuanzisha sheria ya mali isiyoweza kuelezeka kule ilikotoka 2017.

Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ufisadi Transparency International, hivi karibuni lilitaja vifaa vya kimatibabu kukabiliana na virusi vya corona vilivyoagizwa na Zimbambwe kama wenye mashaka.

Shirika hilo lilisema  bei za vifaa vya matibabu ziliongezwa na kuashiria uwezekano wa ufisadi unaoendelea nchini humo.

Waziri wa Afya, Obadiah Moyo alishtakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya mamlaka yake yenye kuhusishwa na kandarasi ya uagizaji wa bidhaa hizo, anatarajiwa kufikishwa tena mahakamani Julai, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles