24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Waislamu Sri Lanka waituhumu Serikali

KOLOMBO, Sri Lanka

JAMII ya Waislamu nchini Sri Lanka, imesema  mamlaka inatumia janga la virusi vya corona kuwatenga kwa kuwalazimisha kuchoma wapendwa wao waliokufa hatua ambayo hairuhusiwi katika dini ya Kiislamu.

Mei 4, mwaka huu, Fathima Rinoza, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 wa watoto watatu kutoka jamii ya Wasilamu waliowachache wa Sri Lanka, alilazwa hospitalini baada ya kushukiwa kuambukizwa virusi vya corona.

Fathima ambaye alikuwa akiishi mji wa mkuu wa Colombo,amekuwa na matatizo ya kupumua na mamlaka ilihofia ameambukizwa ugonjwa wa Covid-19.

Siku aliyolazwa hospitali, mume wake, Mohamed Shafeek alisema mamlaka ilimtenga mkewe na familia yake.

“Polisi, jeshi  na maofisa walikuja nyumbani kwetu hadi mlangoni,” anasema. “Tulirushwa nje na wakanyunyiza dawa kila sehemu. Sote tuliogopa, hawakutuambia chochote. Hata mtoto wa miezi mitatu alipimwa kama  ana virusi na walituchukulia kama mbwa hadi eneo la karantini,”alisema.

Familia hiyo, ilizuiliwa kwa usiku mmoja,ikatolewa siku iliyofuata na wakatakiwa kujifungia kwa wiki mbili.

Wakati huo walikuwa wamepokea taarifa kwamba Fathima amekufa hospitalini,tulilazimishwa kusaini makaratasi

Kijana mkubwa wa Fathima, alitakiwa kwenda hospitali kutambua mwili wa mama yake. Akaambiwa hawezi kuruhusiwa kurejea kwenye familia kwasababu kifo cha mama yake, kimehusishwa na ugonjwa corona.

Alisema alilazimishwa kusaini makaratasi ili kuruhusu mwili wa mama yake kuchomwa moto hata inadawa chini ya sheria za Kiislamu, kuchoma moto mwili wa mwanadamu kama ukiukaji wa dini hiyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles