30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Malawi wapiga kura kuchagua rais leo

LILONGWE, Malawi

WANANCHI wa Malawi, leo wanapiga ya duru la pili ya uchaguzi wa kinyang’anyiro cha kumchagua rais.

Hii imekuja miezi mitano, baada ya  Mahakama ya Kikatiba kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka jana uliokumbwa na utata.

Rais aliye madarakani Peter Mutharika, alitangazwa mshindi Mei, mwaka jana,baada ya kupata ushindi mdogo wa asilimia 38.5 ya kura zote zilizokuwa zimepigwa.

Lakini viongozi wa upinzani walipinga matokeo hayo mahakamani, wakidai uchaguzi  ulikumbwa na udanganyifu.

Majaji walikubaliana nao na kutupilia mbali matokeo hayo Februari na kuagiza marudio.

Kwa sasa upinzani umeungana na kutoa mgombea mmoja ambaye atakabiliana na Rais Mutharika – anayewania muhula wa pili madarakani.

Kwa miezi kadhaa sasa, raia wa Malawi wamekuwa katika mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo. Ni zaidi ya mwaka sasa tangu mamilioni ya raia walipojitokeza katika uchaguzi wa bunge na urais.

Lakini katika uchaguzi wa leo, nchi hiyo imegawanyika vikali. Kumekuwa na maandamano ya kupinga Serikali pamoja na kutokea kwa ghasia ambako kumetishia nchi kutumbukia katika mgogoro mkubwa zaidi.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Malawi,amejiuzulu huku wanachama wapya wa tume  wakichaguliwa ili kusimamia uchaguzi huo.

Uchaguzi huu, ni kinyanganyiro kati ya Rais Mutharika dhidi ya mpinzani wake, Lazarus Chakwera, aliyekuwa mwinjilisti  ambaye ameunganisha upinzani chini ya muungano ambao unaonekana kuwa tayari kukabiliana na Chama tawala cha Democratic Progressive ambacho kiliundwa 2004 na kaka yake rais wa sasa.

Uchaguzi huu pia unafanyika chini ya sheria tofauti, baada ya mahakama kutoa uamuzi mfumo wa chaguzi zilizopita (anayepata kura nyingi hata kama hajafikisha asilimia hamsini ya kura zilizopigwa anatangazwa mshindi) ulikuwa kinyume na katiba.

Atakayeibuka na ushindi kati ya wagombea hao wawili, atakuwa na kibarua kigumu cha kukabiliana na mgawanyiko uliojitokeza na kumaliza ghasia ambazo zimekuwa zikishuhudiwa katika kipindi cha mwaka moja uliopita.

Kukabiliana na ufisadi, kupunguza umaskini na ukosefu wa ajira ni miongoni mwa masuala ya msingi katika uchaguzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles