30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

RC aagiza aliyetapeli fedha waganga wa jadi achunguzwe

NA Mwandishi Wetu- Tabora

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ameagiza kurudishwa kwa ofisa mtendaji wa kata aliyehamia Ilolangulu kutoka  kituo chake cha zamani cha Igalula wilayani Uyui ili ajibu tuhuma za kukusanya fedha kwa waganga wa jadi na tiba mbadala bila kuwapatia stakabadhi.

Alisema mtuhumiwa, Said Mabuga ametuhumiwa  kukusanya mbalimbali na kuandika katika karatasi ya daftari bila ya kutoa stakabadhi halali ambayo zingeonyesha uhalali wa malipo anayokusanya.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana, akiwa katika Kata ya Igalula wilayani Uyui, wakati wa kuhamasisha wafanyabiashara wadogo kuchukua vitambulisho ili waweze kufanyakazi zao kwa amani.

“Tunataka aandikiwe barua ya kurudi hapa hili aje kujibu tuhumu zilizoelezwa na wananchi hapa ambazo ni kukusanya fedha za wananchi bila ya kuwapa risti…tunaka kujua anakusanya kwa utaratibu upi na zinakwenda wapi,” alisema.

Alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)wilayani humo,lazima ifanyie uchunguzi tuhuma hizo na kama kuna fedha zimechukuliwa kinyume na utaratibu kwa wananchi zirejeshwe na mtuhumiwa achukuliwe hatua zaidi.

 Mganga wa jadi , Miraji Adam alisema kwa maelezo yaliyotolewa ,nao watakiwa kuchukua kitambulisho cha wajasiriamali wadogo kwa gharama za Sh 20,000, lakini pamoja na kufanya hivyo,watendaji wamekuwa wakiwatoza  gharama nyingine.

Alisema gharama ambazo wamekuwa wakitozwa zinafika Sh 105,000 ili kupata kibali ya kuendesha shughuli zao.

Alisema wanatakiwa kulipa Sh 10,000  za mtendaji wa kijiji, Sh 10,000 za mtendaji wa kata kusaini barua ya kuomba leseni, gharama za leseni Sh 35,000 na Sh 50,000 ada ya  halmashauri kwa ajili ya baraza la tiba asili na tiba mbadala.

Alisema fedha hizo, zimekuwa nyingi na kipato chao bado ni kidogo kama walivyowafanyabiashara wengine.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Thomas Masese alisema waganga wa jadi kama walivyo wafanyabiashara wadogo, wanatakiwa kupata kitambulisho hicho ambacho gharama yake ni Sh 20,000.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles