31.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyeomba rushwa Sh mil 2/- kwa aliyempa mimba mwanae afikishwa mahakamani

Nathaniel Limu-Singida

TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Ruswa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, imemfikisha mahakamani Juma Salim kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh milioni 2 kwa mwanaume aliyempa mimba mtoto wake ambaye ni mwanafunzi shule ya sekondari.

Hayo yamesemwa juzi na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida,Adili Elinipenda wakati akitoa taarifa yake ya utekelezaji kuanzia  Julai hadi Septemba mwaka kwa waandishi wa habari.

Mzazi huyo aliomba rushwa ili amtorosha mtoto wake kwa lengo la kuharibu ushahidi.

“Mtuhumiwa alikamatishwa shilingi 200,000 kati ya milioni mbili alizoomba.Tuliweka mtego na bahati nzuri ukanasa kwa ufanisi.Mtuhumiwa Juma anaendelea na kesi yake mahakamani. Na kesi yake imepewa namba CC.5/2019”,alisema Adili.

Alisema wanayo kesi ( namba CC.94/2019) nyingine inayondelea mahakamani.Kesi hiyo  inamhusu Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya ya Iramba, Athumani Mkalimoto.

Alisema Mkalimoto anatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa  kwenye mradi wa maji katika Kijiji cha Merya.  

“Pi tumemfikisha mahakamani Ofisa Mtendaji Kata ya Kitaraka, Gasto Kakiziba kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 600,000 kutoka kwa mwananchi aliyedaiwa kuhamia Kijiji cha Kitaraka pasipo kufuata utaratibu. Kesi hii ni yenye  namba CC.191/2019”,alisema.

Alisema kwa makosa hayo,ni kinyume na kifungu cha 15 (i) na (b) vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Alisema  katika kipindi hicho,walifanikiwa kuokoa Sh milioni 40 zilizolipwa kwa Kampuni ya SUMACO.

Alisema kampuni hiyo, ililipwa zaidi ikilinganishwa na vifaa vilivyowasilishwa katika eneo la mradi.

Katika hatua nyingine, alisema wamefanya ufuatiliaji wa fedha za ruzuku ambazo hutolewa na Serikali kuu katika shule za msingi na sekta mbalimbali.

“Tumefanikiwa kubaini upungufu fedha za baadhi ya ujenzi wa vituo vya afya kulipwa posho kwa watumishi,mafundi wasio na mikataba. Kulipwa fedha na ubora hafifu wa majengo”,alisema,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles