24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola atoa wiki mbili kukabili majambazi

Na MWANDISHI WETU-KIGOMA


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi Mkoa wa Kigoma, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya ya Kibondo   na sehemu nyingine mkoani humo.

Amesema katika kupambana na majambazi hao ambao wanasumbua wananchi wa wilaya hiyo na kukosa amani katika maeneo yao, polisi ifanye operesheni maalumu kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.

Alikuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Community Centre mjini Kibondo jana.

Waziri  alisema  operesheni hiyo pia itaambatana na kutoa onyo kwa watu wasio waaminifu wanaowahifadhi raia wa kigeni ambao wengi wao ni wahalifu.

‘’Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, natoa wiki mbili tu, kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya, fanyeni operesheni y kuwasaka majambazi hawa usiku na mchana mpaka jambazi wa mwisho awe amekamatwa,’’ alisema Lugola.

“Haiwezekani tukasalimu amri kwa majambazi, haiwezekani kunyoosha mikono kwa jambazi  waliopo katika maeneo mbalimbali wa wilaya hiyo   na mkoa kwa ujumla,” alisema.

Waziri   alisema anajua changamoto mbalimbali zinazowakibili polisi ikiwamo ukosefu wa magari lakini aliwataka   wawahi katika  matukio ya uhalifu yanapotokea, kwa kutumia hata pikipiki,

Lugola yupo katika ziara ya kazi Mkoa wa Kigoma kutembelea wilaya zote na kufanya vikao na watumishi pamoja na kuzungumza na wananchi.

Mwisho

Majaliwa: Viwanda 1,596

vimejengwa nchini

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema hadi kufikia Juni, 2018   viwanda 1,596 vimejengwa nchini ikiwa  ni  asilimia 61.4 ya lengo la kujenga viwanda 2,600 hadi Desemba 31 mwaka huu.

Alisema hiyo ni katika kutekeleza  agizo la ujenzi wa viwanda 100 katika kila mkoa.

Aliyasema hayo   Dodomaa  jana alipofungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), kwa niaba ya Rais Dk. John Magufuli.

Majaliwa alisema viwanda hivyo vimejengwa kupitia agizo la Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI kwamba kila mkoa ujenge viwanda 100.

Alisema tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali kuelekea uchumi wa viwanda, inaonyesha  mpaka sasa  hekta 367,077 zimetengwa katika mamlaka za serikali za mitaa kwa ajili ya viwanda vikubwa, viwanda vya kati na viwanda vidogo.

“Nitoe wito kwenu kwamba mwendelee kupiga hatua nyingine mbele zaidi katika hili, tujue katika hekta hizo zilizotajwa ni kiasi gani kimerasimishwa kwa viwanda vipi, bidhaa zipi zinazalishwa, hali ya miundombinu ikoje na kuna mikakati gani ya kuiendeleza.

“Pia tufahamu ni ajira ngapi zilizozalishwa kutokana na kuanzishwa viwanda hivyo,” alisema.

Aliwaagiza viongozi na wasimamizi wa mamlaka za serikali za mitaa kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu  kuwawezesha wananchi kushiriki  kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo na kuibua fursa za uwekezaji.

Pia kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vikubwa  Tanzania iweze kufikia lengo la kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Tumieni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia vikundi vyao   wawekeze katika viwanda vidogo vidogo vyenye kuleta tija na kuongeza pato la kaya  kuutokomeza umaskini,” alisema.

Waziri Mkuu allisema lengo la Serikali katika Dira ya Maendeleo ya 2025 ni kuhakikisha halmashauri zinakuwa na uwezo wa kujitegemea kwa mapato kwa zaidi ya asilimia 80 ifikapo 2025.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikichukua hatua mbalimbali  kuhakikisha lengo hilo linatimia.

Serikali imeanzisha utaratibu wa kugharamia miradi ya mkakati yenye lengo la kuziongezea halmashauri mapato ya uhakika na kupunguza utegemezi wa ruzuku, alisema.

“Hadi sasa Sh bilioni 131.5 zimeidhinishwa kutekeleza miradi ipatayo 22 katika halmashauri 17 zilizokidhi vigezo kwenye mikoa 10.

“Hivi ninavyozungumza, tayari Sh bilioni 16.4 zimekwisha kupelekwa kwenye halmashauri hizo kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles