Lugha zisizofaa zinazotolewa na baadhi ya wauguzi katika hospitali za serikali zinachangia kwa kiasi kikubwa wagonjwa kukacha kutibiwa katika hospitali hizo.
Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda amesema hayo leo wakati akizindua huduma ya madaktari bingwa mkoani Mtwara na kuongeza kuwa hospitali zinakosa wagonjwa wengi kutokana na madaktari na wahudumu kukosa ukarimu kwa wagonjwa hao.
“Hivi ni kweli wahuduma wa afya hawajui kama wagonjwa ndiyo mtaji wao? Hawa ni mali kuliko mali nyingine wale ambao wanakuwa wanatoza fedha nyingi na watu wanakwenda ni kwa sababu ya ukarimu wao kwa wagonjwa,” amesema Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).