27 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP, KIM JONG-UN WAITANA ‘VICHAA’ SEOUL, KOREA KUSINI

KIONGOZI wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaja kuwa ‘’na matatizo ya kiakili’ yamemwongezea motisha zaidi ya kuendelea kutengeneza makombora ya taifa lake.

Katika taarifa  binafsi isiyo ya kawaida, Kim amesema Rais Trump ‘atalipia kauli’ zake alizotoa wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo alionya ataiangamiza Korea Kaskazini pale Marekani itakapolazimika kujilinda.

Trump naye alijibu akisema kuwa ‘mwenda wazimu’ hajawahi kufanyiwa atakachofanyiwa akijaribu.

Mataifa hayo mawili wamejibizana kwa kurushiana maneno makali katika siku za hivi karibuni.

Rais Kim alimaliza taarifa yake kwa kusema atamnyamazisha kiongozi huyo ”aliye na akili pungufu’ kwa vita.

China ilijibu vita hivyo vya maneno ikionya kuwa hali ni mbaya.

”Pande zote zinapaswa kujikaza badala ya kuchokozana” , alisema msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Lu Kang.

Urusi pia ilitoa wito wa kuvumiliana  na kusema vita maneno ya kitoto baina ya viongozi hao wawili ni kama wanafunzi wa chekechechea.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov alisema kuwa Moscow ina wasiwasi kuhusu kiwango cha wasiwasi kinachozidi kuongezeka.

Korea Kaskazini imekuwa ikifanyia majaribio makombora yake katika kiwango kisicho cha kawaida na kufanya jaribio lake la sita la kinyuklia licha ya vikwazo na shutuma za kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles