29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

SEDUCE ME YAWAKOSHA FIESTA MWANZA

Na MWANDISHI WETU-MWANZA

MSANII wa muziki wa Kizazi kipya nchini, Ali Kiba anayetamba na wimbo wake wa ‘Seduce Me’, amewapagawisha wakazi wa Mwanza waliofurika katika Uwanja wa CCM Kirumba, kushuhudia tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika juzi usiku.

Kiba ambaye alipanda jukwaani na kuimba wimbo huo, ilimlazimu kurudi jukwaani mara tatu kuimba wimbo huo ambao mashabiki walikuwa wakifuatisha kuimba wimbo huo pamoja naye.

Kiba alionyesha umahiri wake wa kuimba wimbo huo pamoja na kucheza na hivyo kuamsha shangwe kwa mashabiki waliofurika katika uwanja huo.

Tamasha hilo la Tigo Fiesta lilifunguliwa na msanii Rosa Ree ambaye alionyesha umahiri wake kwa kuimba nyimbo zake zikiwemo ‘Mchaga mchaga’ na ‘Up in the air’ na kisha kupanda jukwaani msanii Lulu Diva.

Wasanii Roma na Stamina wao walikuja kivingine walipopanda jukwaani, kila mmoja na baiskeli yake na kuweka kitu tofauti kwenye wimbo wao wa ‘Huku ama kule’ na kuwa kivutio kwa mashabiki waliofurika katika uwanja huo.

Pia msanii Ben Pol alipanda jukwaani na kuimba wimbo wake wa Moyo Mashine, huku akisindikizwa na msanii Mau Sama aliyepanda jukwaani kucheza naye na kufanya mashabiki wapige kelele za shangwe.

Wasanii wengine walionogesha tamasha hilo ni Ommy Dimpoz ambaye alizindua wimbo wake mpya wa ‘Cheche’ uliokuwa gumzo pamoja na Rayvanny ambao hawakushiriki matamasha yaliyopita.

Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande, alisema mwaka huu wameamua kudhamini Fiesta ili kusaidia vipaji vya wasanii na kuwaletea wateja wao burudani na kurudisha faida kwa jamii.

Kaulimbiu ya Tigo Fiesta mwaka huu ni ‘Tumekusoma’ na kwamba baada ya wasanii hao kuuwasha moto Mwanza, Ijumaa watahamia Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na burudani hiyo kuendelea katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Dodoma.

Maeneo mengine ambayo Tigo Fiesta itafanyika ni Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara na kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuhusiana na tamasha la mwaka huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Fiesta, Sebastian Maganga, alisema Tigo Fiesta ni burudani ya kipekee ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki na kwamba mashabiki wamefurahia burudani Arusha na wataendelea kufurahia zaidi katika mikoa mingine.

“Tutawaletea wasanii wenye hadhi kulingana na mapendekezo ya mashabiki husika wa mkoa huo, tena wale waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles