29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

FEDERER AYAAGA MASHINDANO YA US OPEN

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA namba tatu kwa ubora wa mchezo wa tenisi duniani kwa upande wa wanaume, Roger Federer, ametupwa nje ya michuano ya US Open baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa Juan Del Potro.

Bingwa huyo raia wa nchini Uswisi mwenye umri wa miaka 36, alikutana na ushindani wa hali ya juu kwenye mchezo huo wa robo fainali na kuupoteza kwa seti 7-5 3-6 7-6 6-4 dhidi ya mpinzani huyo mwenye umri wa miaka 28, raia wa nchini Argentina akiwa anashika nafasi ya 28 kwa ubora wa mchezo huo duniani.

Kutokana na hali hiyo, Del Potro, mchezo wake wa nusu fainali anatarajia kukutana na bingwa namba moja kwa ubora wa mchezo huo, Rafael Nadal.

Del Potro amewashukuru mashabiki wake kutokana na sapoti kubwa waliyoionesha kwenye mchezo huo wa robo fainali na anataka hali hiyo iendelee katika hatua ya nusu fainali dhidi ya bingwa wa dunia.

“Nadhani kuingia nafasi hii imetokana na sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wangu, nilijiona kama nipo kwenye uwanja wa nyumbani, nilikuwa na furaha kila wakati, nadhani nilikuwa katika ubora wangu na ndio maana nimeweza kushinda japokuwa haikuwa kazi rahisi.

“Kwa sasa siwezi kuamini kama nimeingia tena kwenye nusu fainali baada ya kutoka majeruhi ambayo yalinifanya nifanyiwe upasuaji, imani yangu kubwa ni kufanya vizuri katika hatua inayofuata,” alisema Del Potro.

Kwa upande wa Federer, alidai kuwa lengo lake kubwa lilikuwa ni kucheza nusu fainali dhidi ya mpinzani wake Nadal, lakini kumbe kiwango chake kwa kipindi hiki hakikuweza kutosha kuweza kufikia hatua hiyo.

“Najua ushindani kwangu ulikuwa mkubwa sana, lengo langu lilikuwa kufanya vizuri lakini ilikuwa inategemea na wapinzani wangu.

“Ni vigumu kuelezea kile kilichotokea kwa upande wangu, lakini ukweli ni kwamba mpinzani wangu alikuwa bora kwa kutafuta pointi, lakini japokuwa nimetolewa ila ninayo furaha kuweza kufika hatua ya robo fainali, hivyo siwezi kuchukizwa sana kwa kuwa ni hatua kubwa kwenye michezo hii, ila nilikutana na mpinzani ambaye alikuwa bora zaidi,” alisema Federer.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles