24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

INIESTA AKANUSHA KUKUBALIANA BARCELONA

BARCELONA, HISPANIA
KIUNGO wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta, amekanusha taarifa kwamba amefikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo juu ya kuongeza mkataba mpya katika kipindi hiki cha majira ya joto.
Rais wa klabu hiyo, Josep Bartomeu, aliweka wazi kuwa tayari wamefikia makubaliano na mkongwe huyo juu ya kumuongezea mkataba mpya kabla ya mkataba wa sasa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
“Tayari tumekubaliana pande zote mbili juu ya mkataba mpya, tunaamini kila kitu kitakuwa sawa wiki chache zijazo, tunaamini Iniesta soka lake litamalizikia hapa,” alisema Bartomeu.
Iniesta ambaye alikuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania kwenye michuano ya kuwania kufuzu Kombe la dunia, baada ya kuwasili katika klabu yake alikanusha taarifa hiyo ya kumalizana na uongozi huo.
“Hakuna mazungumzo yoyote ambayo nimeyafanya na uongozi wangu juu ya kuongeza mkataba mpya, kila kitu kitakuwa wazi mwishoni mwa msimu huu,” alisema Iniesta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles