27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

DE BOER KUFUKUZWA KAZI WIKI HII

LONDON, ENGLAND

UONGOZI wa klabu ya Crystal Palace, umeweka wazi kuwa upo tayari kumfukuza kazi kocha wao, Frank de Boer, endapo atashindwa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wake wa ligi dhidi ya Burnley Jumapili.

Klabu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo mitatu, katika michezo hiyo iliyochezwa tangu kufunguliwa kwa ligi klabu hiyo imepoteza yote, hivyo uongozi umeamua kumpa kocha huyo mchezo mmoja wa mwisho ili kulinda kibarua chake.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona, akicheza nafasi ya ulinzi, anaamini kikosi chake kipo tayari kucheza na Burnley na kitafanya vizuri na wala hana wasiwasi.

Tayari uongozi huo umeanza mzungumzo na kocha wao wa zamani, Sam Allardyce, ambaye aliwaokoa kutoshuka daraja msimu uliopita, hivyo lengo lao ni kuhakikisha wanaipata saini yake baada ya De Boer kushindwa kulinda kibarua chake.

De Boer mwenye umri wa miaka 47, amesema mipango yake katika mchezo huo ni kuhakikisha anatumia mfumo wa 4-3-3 dhidi ya Burnley, mfumo huo ulimfanya kocha huyo afanye vizuri wakati anaitumikia klabu ya Ajax, hivyo anaamini mchezo wa Jumapili utamfanya afanikiwe kutimiza malengo yake.

Katika michezo mitatu ya ufunguzi wa ligi, Crystal Palace haijafanikiwa kupachika bao hata moja, lakini wao wamefungwa mabao sita.

Kwa upande wa Burnley, wao wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja, hivyo kuwafanya wawe na pointi nne. Mchezo huo wa Jumapili Burnley watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Turf Moor, hivyo wanaamini wanaweza kufanya vizuri mbele ya mashabiki wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles