26 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

MJUMBE WA BODI CUF AVUNJA UKIMYA

Na MWANDISHI WETU-CHAKECHAKE

MJUMBE  mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha wananchi (CUF), Asha Suleiman Said, amesema kila mtanzania ana hiari ya  sheria na  katiba kuchagua  na kuamua kumuunga mkono kiongozi na chama cha siasa anachokiona kinafaa bila kupata kushurutishwa.

Kauli hiyo aliitoa juzi mjini Chakechake kisiwani hapa na kusema amepokea kwa furaha  na heshima kuteuliwa  kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini ya CUF huku wajumbe wote  sasa wakitambuliwa na RITA kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba ya CUF.

“Kwanza niseme nimepokea na kukubali kwa dhati uteuzi wa kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini, mimi ni mwanachama hai mwenye akili timamu   ninayeweza kufanya uamuzi wangu binafsi bila kuingiliwa na mtu.

“Ninachokiamini siasa si dini wala viongozi wake si mtume ya Mungu,” alisema Asha.

Alisema kila binadamu ana uhuru na uamuzi wake binafsi kwa mujibu wa utashi na hiari yake  hivyo binafsi   hawezi kuendeshwa puta au kulazimishwa aunge mkono jambo asilolipenda na kuliafiki.

“Maisha ya siasa ni mapito katika maisha ya dunia, hayupo mwenye daraja ya unabii na  roho ili  lazima aungwe mkono yeye au chama chake.

“Itapendeza sana viongozi wetu  wanaovutana  kwa miezi kadhaa wakakaa pomoja   kumaliza tofauti na kuendeleza chama chetu,” alisema Asha.

Alimsifu Rais Dk. John Magufuli kwa ujasiri na kupenda kwake tabia ya uzalendo huku akipigania maslahi ya umma na kutaka keki ya Taifa igawanywe sawa kwa sawa.

“Tumebahatika kumpata Rais anayejali shida na dhiki za watu, mzalendo na si kibaraka anayepapatikia mabeberu.

“Mtawala huyu ameletwa awaokoe na kunusuru wanyonge dhidi ya wanyonyaji, ninamuunga mkono pia namkubali katika utendaji wake,” alisema .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles