24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo cha Diplomasia chatakiwa kutoa elimu bora

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

CHUO cha Diplomasia Tanzania, kimetakiwa kuzingatia utoaji wa elimu bora yenye kukidhi mahiaji ya dunia kwa maslahi mapana ya Taifa.

Wito huo umetolewa leo Desemba Mosi, jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agnes Kayola katika mahafari ya 24 ya chuo  hicho.

Amesema utoaji wa mafunzo bora kwa wanadiplomasia kutasaidia Taifa kuimairisha mahusiano kimataifa na hatimaye kujenga uchumi imara.

Aidha amewataka wahitimu kutambua kuwa elimu ni ufunguo wa maisha hivyo wakaitumie kufungua mafanikio yao na taifa kwa ujumla.

“Mtumie lugha ya kiswahili  kwa wadau wa ndani na nje ya nchi ilikuongeza utafiti na ushauri elekezi  ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazolikumba Bara la Afrika ikiwamo ugaidi, mabadiliko ya tabia ya nchi, mapigano ya waasi  na uharifu wa bahari,” amesema Balozi Agnes.

Balozi huyo amewapongeza  wanafunzi walihitimu  akiwataka iwe chachu ya kujiendeleza  zaidi na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Abraham Kaniki, amesema chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo kukosa maeneo ya kupeleka wanafunzi kufanya mafunzo kwa vitendo.

Aidha amesema chuo hicho kinawakaribisha wahadhiri na taasisi mbalimbali kuandika makala zitakazochapishwa kwenye jarida linaloandaliwa na chuo.

“Katika kuimarisha maofisa wa serikali na sekta binafsi ili kuendana na mabadiliko yanayotokea duniani, chuo  kimeendesha kozi fupi ambazo ni Diplomasia ya uchumi, Ofisa Uhusiano na Itifaki, Itifaki na uhusiano wa Serikali, usuluhishi wa amani migogoro na amani na zinginezo,amesema.

Amesema wamezalisha  mabalozi 20, waliopangiwa katika mataifa mbalimbali na watumishi zaidi ya 102 wanaofanya kazi katika Wizara ya Mambo Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kikanda waliopangiwa ofisi mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles