26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rufaa ya Mbunge Bukoba Vijijini yatupiliwa mbali

Na Nyemo Malecela, Kagera

MAHAKAMA ya Rufani Kanda ya Bukoba imekubaliana na hoja za Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kwa kutupilia mbali rufaa ya Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini ,Jason Rweikiza ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba  katika kesi ya madai namba 12/ 2016 dhidi ya Mjumbe wa Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Kagera, Novatus  Nkwama kuwa alimdhalilisha na kumuondolea hadhi yake .

Rufaa hiyo ya madai namba 305/2020 ilisikilizwa mbele ya  Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Jaji S.E.A. Mugisha, Jaji W.B. Korosso na Jaji P.F. Kihwelo

Mrufani Jason Rweikiza na mrufaniwa Novatus Nkwama kupinga hukumu ya mahakama kuu kanda ya Bukoba  kesi ya madai namba 12/2016.

Katika kesi hiyo Mbunge wa Bukoba Vijijini Jason Rweikiza alikuwa anadai fidia maalumu ya shilingi milioni 216 na fidia ya jumla shilingi bilioni moja.

Mahakama ya Rufaaa imesema mrufani ni kweli alishindwa kesi kwa sababu ameshindwa kuthibitisha tuhuma za uzalilishaji alizofanyiwa na Novatus Nkwama, hivyo mahakama hiyo imetupilia mbali madai na tuhuma hizo kwa gharama ambapo Jason Rweikiza anatakiwa kulipia gharama za kesi mahakama ya rufani.

Mrufaniwa Novatus Nkwama alikuwa anatetewa na mawakili wawili Jovi Rutainulwa na Dustan Mujaki na upande wa utetezi umesema umeridhishwa na uamuzi wa mahakama ya rufani kwa kutenda haki kwa mteja wako.

Upande wa mrufani Jason Rweikiza alikuwa wakiwakilishwa na wakili Al-Muswadiku Chamani ,alipohojiwa kuhusu maamuzi ya mahakama hiyo alisema hawezi kuzungumza chochote kuhusu kesi hiyo.

Awali Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mkoani Kagera  ilitupilia mbali kesi ya  madai namba 12 ya mwaka 2016  ya fidia ya shilingi bilioni 1 na milioni 216 iliyofunguliwa  na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini  Jasson Rweikiza dhidi ya mjumbe wa halmasahauri ya chama cha mapinduzi (CCM )Mkoa wa Kagera Novatus  Nkwama kuwa alimdhalilisha.

Akisoma hukumu mahakamani  hapo, Jaji wa mahakama hiyo Dk.Ntemi Kilekamajinga ,alidai kuwa baada ya kuzingatia ushahidi wa pande zote mbili kwanza msingi wa kisheria  ni wajibu mdai kuthibitisha madai yake mahakamani.

Jaji Dk.Kilekamajinga, alisema katika kesi hiyo aliangalia hoja nne za kesi hiyo ambavyo ni ambazo ni Je mdaiwa alimdhalilisha  mdai?

 Pili ni maneno yaliyosemwa yalikuwa na udhalilishaji? Tatu ni je maneno hayo yalisababisha madhara yoyote ya udhalilishaji? Na nne maneno ya kushusha hadhi kwa jamii yajulikane na mtu zaidi ya mmoja.

“Nimechambua ushahidi uliotolewa na mdai yeye hakuwahi kuyasikia maneno ingawa alisikia kupitia kwa watu wakati huohuo anasema alisikia kipindi kikirudiwa katika radio, anasema kama yeye hakusikia kupitia masikio yake ushahidi wake unaleta ukakasi,” alisema  Jaji dk.Kilekamajinga.

Amesema kifungu cha 62 kifungu kidogo cha (1)cha sheria za ushahidi alitakiwa kuijumuisha Radio karagwe kwenye ushahidi mahakamani hapo.

Ameeleza mahakama kwamba mdai hakumpeleka mahakamani mtangajazo wa radio hiyo ,wala uthibitisho wowote toka radio karagwe kwamba ilirusha matangazo yaliyomdhalilisha.

Amesema kuhusu madai kuwa Rweikiza alitukanwa kwenye nyumba ya Nazir Karamagi wakati wa dua mtu anaalikwa kusalimia halafu anaanza kuropoka na kuanza kutukana hilo jambo pia linaleta ukakasi. 

Amesema shahidi mwingine wa mdai aliieleza mahakama kuwa akiwa njiani kuelekea Bukoba Mjini alipita Itawa akasikia mdaiwa anamtukana mdai, sijui kilichomsimamisha kwa kweli sasa nimejiuliza alitumia usafiri gani kwanza hakuwa pale na ajenda ilikuwa moja ya kujadili wizi katika Kitongoji pia ushahidi wale ni wa ukakasi. 

Amesema mashahidi waliieleza mahakama  kuwa waliacha kazi kwa mdai baada ya kusikia maneno ya udhalilshaji  walishindwa kuithibitishia mahakama kama kweli waliacha kazi na hawakuleta barua.

Amesema mdai alishindwa kuithibitishia mahakama madai yake ya watoto 50 wa kiislamu waliokuwa wanasoma kwenye shule yake ya ( Rweikiza primary school).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles