24.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ama’z yadhamiria kufanya makubwa sekta ya udalali

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Udalali ya Ama’z imesema imedhamiria kutoa huduma bora na yenye manufaa kwa jamii na kuzingatia uaminifu na uadilifu.

Kampuni hiyo iliyoanzishwa Julai mwaka huu,inajishughulisha kukusanya kodi na ushuru, kudai madeni, kuuza vitu mbalimbali kama vile nyumba, viwanja, samani, kufanya minada, kupangisha, kuratibu safari za kitalii, kukusanya taka hatarishi na kutao ushauri wa kiufundi.

Akizungumza leo Desemba Mosi,2021 wakati wa kuitambulisha kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ama’z, Dawa Jumanne, amesema wanafanikisha biashara na huduma mbalimbali sehemu za mjini na vijijini.

Amesema pia wanatarajia kufungua matawi katika kila kanda hapa nchini pamoja na kujitanua nje hasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Tunashukuru katika kipindi cha muda mfupi tangu tuanzishe kampuni yetu tumepokelewa vizuri kwani baadhi ya taasisi za Serikali, taasisi binafsi na watu mbalimbali wametupa ushirikiano mkubwa,” amesema Dawa.

Amewashauri wateja kutafuta madalali ambao wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria ili yanapojitokeza matatizo yanayohusiana na shughuli za udalali wawe na haki ya kisheria.

“Tunawakaribisha wenye kampuni, taasisi na wananchi mbalimbali walioko ndani na nje ya nchi wanaotaka kuuza au kununua vitu mbalimbali waitumie kampuni yetu,” amesema Dawa.

Aidha amesema hata wanapopata kazi za kudai madeni huwa hawatumii nguvu kubwa bali hushauriana na mdaiwa husika na kama ikishindikana ndivyo wanachukua hatua zingine.

“Hatutumii nguvu kubwa kudai madeni tunatafuta suluhu kwa kuzungumza na mdaiwa husika na pale tunapoona imeshindikana ndiyo nachukua hatua zingine.

“Tunawashauri watu wanaodaiwa kama na taasisi za fedha wakiwa na matatizo wasikae kimya wawe wazi na kuzieleza taasisi husika kwa sababu ukikaa kimya riba inazidi kuongezeka,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema pia hadi sasa kampuni hiyo imetoa ajira kwa zaidi ya vijana 200 kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles