27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wanamipango wakumbushwa majukumu yao

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WIZARA ya Fedha na Mipango imewataka wanamipango nchini kuhakikisha wanapanga na kusimamia vema utekelezaji  wa mipango ya maendeleo kwa kutekeleza na kutatua changamoto mbalimbali ikiwamo ya ukosefu wa ajira.

Hayo yameelezwa leo Desemba Mosi,2021 jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Adolf Ndunguru wakati akifungua kongamano la wanamipango la mwaka 2021 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Emmanuel Tutuba.

Ndunguru  amesema kuna changamoto mbalimbali  kama ukosefu wa ajira  kwa vijana,athari za mabadiliko ya tabia nchi,umaskini na maradhi mapya ya UVICO 19.

“Kama wanamipango  tunajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa tunapanga na kusimamia vema utekelezaji  wa mipango ya maendeleo kwa kuweka na kutekeleza vipaumbele vya kutatua changamoto hizo,”amesema.

Ndunguru ametoa rai kwa wanamipango wasichoke kutoa ushauri na mapendekezo kwa Serikali kwa lengo la kuboresha utekelezaji wa majukumu ya msingi na kuendeleza kada ya wanamipango.

“Natoa rai kwa wanamipango wote popote walipo kuendelea kuenzi nia njema ya Serikali  kwa kufanya kazi kwa bidii weledi na uadilifu mkubwa,”amesema.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema wizara inaahidi kuyafanyia kazi maazimio yote ambayo watakubaliana huku akiwasihi kuwa mabalozi wazuri wa kongamano hilo.

“Dhima ya kongamano hili ni ‘Mwanamipango Imara kwa Ustawi wa Taifa’ dhima hii imezingatia jukumu kubwa lililo mbele yetu la kuibua, kupanga, kutekeleza, kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa za utekelezaji wa mipango ya maendeleo,”amesema.

Akimkaribisha mgeni rasmi,Kamishna Msaidizi Idara ya Mipango ya Kitaifa,Wizara ya Fedha na Mipango,Ekingo Magembe amesema wanamipango wanajukumu la kuandika maandiko mazuri ambayo yatasaidia nchi kuweza kupata maendeleo.

“Tukiwa katika mchakato wa kuandaa dira ya 2025 ni lazima muongezewe uwezo wa namna bora ya kuandika maandiko pamoja na namna ya kuwa bora,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles