27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yanadi vivutio vya utalii Madrid

Na Mwandishi Maalum, Madrid, Hispania

UJUMBE wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro upo Jiji la Madrid nchini Hispania, kushiriki mkutano mkuu wa 24 wa Kimataifa wa Utalii Duniani ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa  linaloshughulikia masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO), huku ukitumia fursa hiyo kunadi vivutio vya Tanzania.

Katika mkutano huo wa siku nne ulioanza jana Novemba 30,unaotarajiwa kufunguliwa  rasmi leo Desemba Mosi, ambapo Waziri Ndumbaro ameweka bayana mambo mbalimbali ambayo Tanzania itanufaika na mkutano huo.

Akizungumzia mambo hayo, Dk. Ndumbaro amesema  katika  kuhakikisha idadi ya watalii inaongozeka pamoja na mapato yatokanayo na Utalii, suala la kutangaza utalii wa Tanzania katika nyanja za kidunia ni suala ambalo haliepukiki.

Ametaja moja ya kati ya maeneo ya  kutangaza utalii huo, ni kuhudhuria mikutano mikubwa duniani  ikiwamo kwenda Hispania ambako ndiko makao makuu ya utalii duniani  katika jiji la Madrid kwa ajili ya  kuhudhuria mkutano.

Ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano huo, Tanzania ilipata fursa ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro ( katikati) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi ( kulia)  wakipewa maelezo ya namna ya kujisajili  mara baada ya  kuwasili kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 24 wa Kimataifa wa 24 wa  Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii  linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) ulioanza leo katika Jiji la Madrid nchini Hispania, Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Ufaransa, Samwel Shelukindo

”Waje Tanzania wauone Mlima Kilimanjaro, waje Tanzania waione Serengeti, waje Tanzania waione Ngorongoro, waje Tanzania waone fukwe nzuri zenye mchanga mweupe zilizopo Zanzibar, waje Tanzania waone vivutio mbalimbali ambavyo tupo navyo.’’ Amesema Dk. Ndumbaro.

Dk. Ndumbaro amesema jambo la   pili katika mkutano huo, Tanzania itasaini mkataba na UNWTO wa kuweza kuwa mwenyeji wa mkutano wa 65 wa Utalii Barani Afrika ambao utafanyika kati ya tarehe 6-8 Oktoba 2022 katika jiji la Arusha.

‘’Mkutano huu tunauleta kwa sababu ni fursa nyingine kwa  Tanzania, Tulishapewa kuwa mwenyeji wa mkutano wa utalii wa kanda ya Afrika  kule nchini Cape Verde, lakini sasa tumekuja kusaini makubaliano ya kuwa wenyeji wa  mkutano huo, baada ya kusaini sasa tutakuwa na uhakika asilimia 100 na tumetengeneza ‘Post card’ ambapo kila mshiriki aliyekuja hapa tunampa post kadi hizi ambayo inasaidia sana kutangaza utalii wa Tanzania.

‘’Jambo lingine ambalo tunalifanya katika mkutano huu, ni kupitisha sheria ya kutetea haki za watalii duniani pale inapotokea matatizo. Tumejifunza kutokana na kadhia ya Uviko- 19 kwamba nchi zilifunga mipaka na baada ya nchi kufunga mipaka, watalii walikuwa wapo  kwenye nchi zingine na hawaweza kurudi.

‘’Sasa haki zao zilikuwa haziwezi kutetewa na sheria za kimataifa. Kwa hiyo sasa tunapitisha sheria ya kimataifa ya kutetea watalii katika mazingira ya dharura kama hayo. Ni sheria ambayo itaongeza heshima ya baishara ya utalii duniani kwa sababu unapolinda haki ya mtalii, mtalii anajiona yupo salama zaidi kuja na kushiriki katika  nchi yako, Tanzania tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha sheria hiyo inapita.’’ Amesema Dk. Ndumbaro.

Amefafanua kuwa mkutano huo una faida nyingi kwa nchi katika kutimiza idadi ya watalii milioni tano na mapato zaidi ya bilioni sita. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles