28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

102 wafutiwa matokeo ya kidato cha nne

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limefuta matokeo ya watahiniwa 102 wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2023 kutokana na udanganyifu na waliondika lugha ya matusi kwenye karatasi za majibu.

Matokeo ya kitado cha nne yametangazwa leo Januari 25, 2024 jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk.Said Mohamed.

Amesema kati hao waliofutiwa matokeo, watano waliondika matusi.

Aidha amesema matokeo ya wanafunzi 376 yamezuiwa kutokana na kupata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani.

Dk.Mohamed amesema watahiniwa walioshindwa kufanya mtihani huo mwaka jana wamepewa fursa ya kufanya masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.

Dk. Mohammed amesema jumla ya watahiniwa 572,359 walisajiliwa kufanya mtihani huo Novemba 2023 ambapo 484,823 sawa na asilimia 87.65 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la ufaulu.

Amesema wasichana waliofaulu ni 257,892, wavulana wakiwa 226,931, huku masomo ya lugha ikiwamo kichina yakifanya vizuri zaidi.

Amesema wanafunzi waliofaulu masomo ya kiswahili asilimia 96.80 na kichina ni 91.36.

“Kati ya watahiniwa 471,427 waliofaulu, wasichana ni 250,147 sawa na asilimia 88.11 na wavulana ni 221,280 sawa na asilimia 90.81. Hivyo, wavulana wamefaulu vizuri zaidi kuliko wasichana,” amesema.

Hata hivyo NECTA imezipongeza Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Halmashauri, Manispaa na Jiji, wakuu wa shule, wasimamizi na wasahihishaji wa mtihani huo kwa kazi nzuri ya kutekeleza jukumu la uendeshaji mtihani huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles