24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wingu zito mabilioni NIDA

Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam*Matumizi ya bilioni 179.6/- hadharani

*Kila kitambulisho chatafuna Sh 89,800
Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

WINGU zito limetanda ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu matumizi ya  Sh bilioni 179.6 ambako kila kitambulisho  cha taifa kimegharimu Sh 89,800 zikiwamo gharama za utawala, MTANZANIA limebaini.

Hayo yamebainika  siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kushangazwa na watendaji wa mamlaka hiyo ikizingatiwa vitambulisho vilivyokwisha kutengenezwa hadi sasa havifiki   milioni mbili na havina saini.

“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina.  Wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana  wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.

“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara wa Sh milioni 35 kwa mwezi…naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.

Rais Dk. Magufuli, licha ya kushangazwa na hali hiyo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilipewa Sh bilioni 70 lakini iliweza kutengeneza vitambulisho   23,253,982 ambavyo vilikuwa na saini ya kila mpiga kura na kila kimoja kimegharimu Sh 3,010.

Kutokana na hali hiyo, tofauti ya gharama kati ya kitambulisho kimoja cha NIDA na cha NEC ni Sh 86,790.

Pamoja na hayo, hivi sasa Watanzania wanasuburi   ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad, kuhusu  matumizi ya fedha hizo za NIDA.

Januari 26 mwaka huu, Rais Magufuli alitangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu.

Maimu alisimamishwa kazi pamoja na maofisa wengine wanne, kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

Akitangaza uamuzi huo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alisema taarifa zilizomfikia Rais zinaonyesha kuwa NIDA hadi wakati huo ilikuwa imetumia Sh bilioni 179.6, kiasi ambacho ni kikubwa.

Alisema Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi kujua jinsi fedha hizo zilivyotumika, maana amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Licha ya kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, afanye ukaguzi maalumu wa hesabu za NIDA  ukiwamo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa, pia aliitaka Takukuru ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

Historia ya NIDA

Mradi wa Vitambulisho vya Taifa umekuwa na historia ndefu. Ulibuniwa mwaka 1972 ikiwa ni  zaidi ya miaka 38 iliyopita kwa kupitisha bungeni Sheria ya Vitambulisho na Uraia ya mwaka 1972.

Tangu wakati huo, mawaziri   waliopita Wizara ya Mambo ya Ndani waliukuta na kuuacha kutokana na sababu mbalimbali  ikiwamo mgongano wa masilahi ya umma na ya binafsi.

Oktoba 1999 mradi huo ulitangazwa na kampuni 27 za nje na ndani ziliomba kazi hiyo. Kutokana na mizengwe, urasimu na hila za ufisadi makampuni 22 yalijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na zabuni ikafutwa katika mazingira ya kutatanisha.

Serikali iliipa kazi hiyo kampuni ya Gotham International Ltd inayomilikiwa na Jack Gotham aliyekuwa akishirikiana na Ofisa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), John Kyaruzi, ambaye alisaidia kuiunganisha kampuni hiyo na Business Connections ya Afrika Kusini na kwa pamoja wakashughulikia ‘mchanganuo’ wa mradi huo.

Mabilioni yanavyopotea

Ripoti mbalimbali zinaonyesha  Serikali imepoteza karibu  Sh bilioni 500 kwa   miaka tisa  kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma  ikiwamo rushwa na ubadhirifu wa mali mbalimbali.

Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia  katika moja ya ripoti zake alizowahi kuzitoa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba.

“Katika kipindi kisichozidi miaka tisa kumeripotiwa kashfa kubwa nne ambazo kwa ujumla wake zimelisababishia Taifa hasara ya karibu Sh bilioni 500 ambako kwa wastani inapoteza takriban asilimia 20 ya bajeti yake ya mwaka,” alisema Sungusia.

Alizitaja kashfa hizo kuwa ni   mabilioni ya shilingi kupitia ununuzi wa rada iliyotumika kutoka Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza, wizi wa mabilioni katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT) na kashfa ya mabilioni ya fedha walizogawiwa baadhi ya viongozi wa uuma, kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles