29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

WFP: Zinahitajika fedha zaidi kufanikisha operesheni Msumbiji

WFP imesema ili mpango wao wa kupanua wigo wa huduma uweze kufanikiwa hadi mwezi Juni, wanahitaji dola milioni 130, huku ikishukuru wahisani ambao tayari wamejitolea kufanikisha operesheni za awali nchini Msumbiji kufuatia kimbunga Idai.

Ili kufanikisha operesheni zake, WFP ilipeleka helikopta tatu za usafirishaji, ndege moja pamoja na magari mawili yanayotembea kwenye maji ambayo yana uwezo wa kubeba tani 1000 za mzigo kama vile chakula na kufikisha maeneo ambayo hayafikiki kwa barabara.

Kwa mujibu wa Karin Manente ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Msumbiji, anasema WFP limesema limeweza kufikisha msaada wa chakula kwa watu milioni mmoja huku likiendelea kupanua wigo wa msaada na kuwapatiwa wananchi misaada ya kujikwamua. 

 “Sasa tumefanikiwa kuwafikia watu milioni moja , hayo ni mafanikio makubwa sana kwetu, na muhimu sana kwa watu wa Msumbiji ambao ndio waathirika wakubwa wa kimbunga IDAI,” alisistiza Manente

Tayari WFP imesambaza wataalamu wa lishe kwenye majimbo manne muhimu ambapo wanaanza kutoa matibabu dhidi ya utapiamlo na mpango ni kutibu takribani watoto na wanawake 100,000 katika kipindi cha miezi sita.

WFP imesema inawapatia wahusika mgao wa siku 30 wa mchele pamoja na unga wa mahindi, maharagwe, vyakula vilivyoongezewa virutubisho pamoja na mafuta.

Pia imesema kwa kuzingatia kiwango kikubwa cha uharibifu uliotokea tangu kimbunga Idai kipige Msumbiji,  mipango ya kuhakikisha Msumbiji inajikwamua itakuwa ni muhimu.

Ni kwa mantiki hiyo, shirika hilo lijitahidi kuhakikisha kuwa tathmini kubwa inayoongozwa na serikali kwa ushirikiano na Benki ya Dunia inaanza wiki hii ili kupatia nchi hiyo mipango bora zaidi ya lishe, chakula na uhifadhi wa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles