27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 150 hawajulikani waliko baada ya boti kuzama Ziwa Kivu

Takriban watu 150 wametoweka baada ya boti walilokuwa wakisafiria kuzama katika ziwa Kivu lilopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

”Nimehuzunishwa na kuzama kwa boti hiyo tarehe 15 mwezi Aprili katika ziwa Kivu. Hadi kufikia sasa idadi ya watu ambao hawajulikani waliko ni 150” , alisema rais wa taifa hilo Felix Tshisekedi katika akaunti yake ya Twitter.

Kulingana na mwanaharakati mmoja katika eneo la Kivu kusini ambaye alikuwa akizungumza na shirika la habari la Reuters, boti hilo ambalo lilikuwa limetoka katika mkoa jirani wa Kivu kaskazini lilizama katika ziwa hilo karibu na eneo la Kalehe.

Alisema kuwa miili mitatu iliopolewa , watu 33 wakaokolewa huku abiria wengine 150 wakiwa hawajulikani waliko kufuatia ajali hiyo.

Tshisekedi amesema kuwa anaifuatilia kwa karibu hali hiyo ili kuwatambua na kuwachukulia hatua wale waliohusika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles