33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

WENYE NGOZI KAVU, MIKUNJO TUMIENI FENESI

Na HERIETH FAUSTINE,

FENESI ni tunda la mti lililo kubwa kuliko matunda mengine ambalo hupatikana kati ya Oktoba mpaka Januari.

Mti wake unaweza kuzaa matunda 100 hadi 200 kwa mwaka huku kila moja likiwa na ujazo wa kilogram 36.

Ni tunda lenye sukari nyingi ambayo huwavutia watu na kupenda kulitumia zaidi.

Asili ya tunda hili ni kutoka nchi ya India ingawa kwa sasa mti wa mfenesi hupandwa mahali penye ukanda wa kitropiki ambapo mvua hunyesha kwa kiasi.

Licha ya kuwa ni tunda tamu, pia mbao za mti wa mfenesi ni nzuri kwa utengenezaji wa fenicha mbalimbali.

Mbao za mti huo ni nzuri kwa utengenezaji wa fenicha mbalimbali.

Kama yalivyo matunda mengine, tunda hili pia lina sodium kilichopo mwilini jambo ambalo huchangia kuongezeka kwa kiwango cha msukumo wa damu mwilini.

Pia madini ya Potassium husaidia kuimarisha mishipa ya moyo.

Licha ya kuwa na madini ya Potassium, pia tunda hilo lina virutubisho vya vitamin A, C na B6 pamoja na madini ya Calcium na Magnesium.

Vile vile tunda hili ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambazo ni muhimu kwa upande wa umeng'enyaji wa chakula na hivyo kumsaidia mhusika kuepukana na shida ya kukosa choo mara kwa mara.

Moja ya kazi nzuri ya fenesi ni kuimarisha kinga za mwili, lakini pia tunda hili huongeza vitamin C mwilini ambayo husaidia seli za damu kufanya kazi vizuri.

Kwa upande wa urembo, tunda hili huwasaidia wale wenye ngozi ya  mikunjo mikunjo, ukitumia fenesi litakusaidia katika hilo na kuondoa ukavu wa ngozi.

Kwa wale wenye shida ya upungufu wa damu yaani anemia tunda hili ni zuri  kwao kutokana na kuwa na madini ya chuma 'iron' ambayo kwa kiasi kikubwa husaidia uzalishaji wa seli nyekundu za damu mwilini.

Matumizi ya fenesi husaidia kuongeza uoni mzuri kutokana na kuwa na vitamin A ambayo ni muhimu kwa afya ya macho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles