29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wengi wajitokeza kuhakiki silaha Dar

NA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

IDADI kubwa ya wakazi wa Jiji wa Dar es Salaam wamelazimika kuacha silaha zao vituo vikuu vya polisi vya wilaya za Kinondoni, Temeke na Kituo cha Kati (Central Police) kwa ajili ya kukaguliwa.

Kuachwa kwa silaha hizo kumesababishwa na muda wa ukaguzi kuisha juzi na hivyo kupewa maelekezo na maofisa wa polisi kuziacha kwenye vituo hivyo mpaka zitakapokaguliwa.

Kazi ya ukaguzi wa silaha kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ilianza mwezi Machi, mwaka huu na ilifikia kikomo juzi Juni 30.

Gazeti hili lilishuhudia umati mkubwa wa watu wakiwa kwenye foleni wakisubiri kuitwa kwa ajili ya kwenda kukaguliwa silaha zao.

Taarifa kutoka kwa maofisa wa polisi wa kituo cha kati waliokuwa wakizungumza na watu waliokuwa wakisubiriwa kukaguliwa silaha zao zilieleza kuwa kazi hiyo imeshindwa kumalizika katika muda uliopangwa kwa sababu ya idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwa ajili ya ukaguzi huo.

“Kule Kinondoni, Temeke na hata hapa watu walikuwa wengi sana kiasi kwamba ilipofika saa moja na nusu ilibidi waambiwe waziache silaha zao na waandike majina yao ili kesho (jana) wafike wamalizie uhakiki wao,” alisikika akisema askari huyo.

Alieleza zaidi kuwa kazi hiyo ya uhakiki wa silaha ilitarajiwa kumalizika jana jioni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles