31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Chalamila awaita wananchi Dar kujitokeza kwa wingi kupiga kura, vituo vyaongezwa

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila amesema vituo vya kupiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa vimeongezwa na kuwataka wananchi waliojiandikisha kutumia fursa ya kukuza demokrasia kwa kuchagua viongozi wanaowahitaji.

Mkoa huo una mitaa 564 na kulingana na taarifa za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 idadi ya watu ni milioni 5.3.

Akizungumza leo Novemba 25,2024 na Waandishi wa habari amesema wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la mkazi yalitokea malalamiko kwamba baadhi ya vituo vilikuwa mbali hivyo walikaa na wadau wa siasa na kuongeza vituo.

“Rais anahitaji uchaguzi uwe huru na haki unaoakisi 4R ambazo ameziasisi, Rais anahimiza kujenga ustahimilivu na kuepuka siasa za chuki hivyo, wananchi watumie uchaguzi huu kutuma salamu kwa mataifa mbalimbali kwamba sasa Tanzania imeiva kidemokrasia,” amesema Chalamila.

Aidha amesema hali ya usalama katika mkoa huo iko vizuri na kuonya kuwa yeyote atakayejaribu kuharibu amani atashughulikiwa.

Akizungumzia jengo lililoanguka Kariakoo hivi karibuni amesema zoezi la uokoaji bado linaendelea na kwamba hivi karibuni wafanyabiashara walio pembezoni mwa eneo hilo watapata taarifa ya kina kuhusu mwenendo wa uokoaji na lini maduka yatafunguliwa.

Jengo hilo lilianguka Novemba 16,2024 na kuua watu 20 huku wengine zaidi ya 80 wakijeruhiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles