33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jengo la Mahakama ya mafisadi laandaliwa

NA MANENO SELANYIKA, DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, amesema ukarabati wa jengo la mahakama maalumu kwa ajili ya kushughulikia kesi za mafisadi utaanza Jumatatu.

Amesema mkandarasi aliyeteuliwa kukarabati jengo hilo atakabidhiwa eneo la mradi ambalo ni jengo la Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, lililoko Chuo cha Sheria, Ubungo, Dar es Salaam Jumatatu.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwasajili mawakili wapya 623, iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Jaji Othman alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria iliyopitishwa na Bunge.

“Muswada wa Sheria umeshapitishwa na Bunge, hivyo karibuni utakwenda kwa Rais Dk. John Magufuli kwa ajili ya kuusaini ili utangazwe kuwa sheria katika gazeti la Serikali kabla ya kuanza kutumika rasmi.

“Jumatatu mkandarasi atakabidhi jengo la mahakama hiyo lililoko katika Chuo cha Sheria, Ubungo ambapo kuna marekebisho yatafanyika kabla ya kuanza kutumika,” alisema Jaji Othman.

Alisema mahakama ina wafanyakazi wa kutosha kutenda shughuli zote za kimahakama na imekwishateua majaji ambao watapewa semina maalumu ya utendaji kazi katika mahakama ya mafisadi.

Aidha, alisema usajili mpya wa mawakili 623 imeongeza idadi ya waliokuwepo hadi kufikia 5,800 na kwamba mawakili wapya waliosajiliwa wanatoka sekta binafsi, serikalini, taasisi na mashirika ya umma na walimu wa sheria katika vyuo vikuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles