BAGHDAD, IRAK
WAZIRI Mkuu wa Irak, Haider al Abadi amemsimisha kazi Waziri wa Nishati Qassim al-Fahdawiz kutokana mgogoro wa nishati ya umeme na huduma mbaya.
al-Abadi ameandika hayo kwenye akaunti yake ya Twitter jana akisema hatima ya kusimamishwa kazi kwa waziri wake huyo itafahamika mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Licha ya mabilioni ya dola kutumika kwenye sekta ya umeme Irak tangu mwaka 2003 baada ya majeshi yaliyoongozwa na Marekani kumg’oa madarakani Saddam Hussein, miji mingi na maeneo ya vijijini, Iraq bado inakabiliwa na upungufu zilizotokea katika jimbo la Basra lenye utajiri wa mafuta.