WAZIRI wa Ulinzi wa Kazakhstani, Nurlan Yermekbayev, amejiuzulu, na hatua hiyo inatokana na tukio la moto na milipuko iliyojitokeza kwenye kambi ya jeshi na kuua wanajeshi 15.
Taarifa ya Yermekbayev kuachia ngazi imetolewa na Ofisi ya Rais wa nchi hiyo ya Asia, Kassym-Jomart Tokayev.
Katika tukio hilo la Agosti 26, mwaka huu, mamlaka zililazimika kuwahamisha wakazi wa eneo la karibu na kambi hiyo, huku chanzo cha moto kikiwa haijafahamika.
Hata hivyo, tukio hilo lililotokea katika Jimbo la Zhambyl lililoko Kusini mwa Kazakhstani, si la kwanza nchini humo, ikikumbukwa kuwa lilikuwapo lililoua watu wanne mwaka 2019.