29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Konta aishia njiani US Open

MKALI wa tenesi kwa upande wa wanawake, Johanna Konta, amelazimika kujitoa kwenye michuano ya US Open kutokana na maumivu ya nyama za paja za mguu wake wa kushoto.

Konta raia wa Uingereza, alifanya uamuzi huo saa chache tu kabla ya kuingia mzigoni kucheza mechi yake ya raundi ya kwanza dhidi ya Kristina Mladenovic wa Ufaransa.

Kutokana na hali hiyo, ilibidi nafasi yake ichukuliwe na bibiye anayeing’arisha Urusi kwenye ulimwengu wa tenesi, Kamilla Rakhimova.

Hili ni pigo jingine kwa bibiye huyo mwenye umri wa miaka 30 kwani hivi karibuni alishindwa kushiriki mashindano ya Wimbledon na Olimpiki baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles