32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wahimizwa kuwapatia elimu bora watoto wao

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SHULE ya Green Harvest Pre and Primary ya Dodoma imesema imejipanga kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu kwa kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa vitendo ili kuwasaidia waweze kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Desemba 9,2021 na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Leticia Ombay wakati akizungumza katika mahafali ya pili ya shule hiyo.

Mkuu huyo wa shule amesema kiujumla hali ya kitaaluma ni nzuri shuleni hapo ambapo amedai wameendelea kufanya vizuri kwa miaka mitatu mfululizo na wanaendelea kufanya vizuri.

“Hii ni kufanya watoto wetu wawe imara na kufanya waongoze juhudi katika masomo. Wanafunzi wanaofanya mahafali walianza mwaka 2019 wakiwa 9 leo utawakabidhi wakiwa 18 kuongezeka kwao ni kutokana na maboresho ya kitaaluma na huduma nzuri zinazotolewa na idara zote katika shule yetu,”amesema Leticia.

Amesema shule hiyo inajivunia ni uwepo wa walimu mahiri wenye sifa na vigezo pamoja na kuwa na kituo cha mitihani kutoka Baraza la Taifa la Mitihani,ambapo amedai wameweza kusajili darasa la nne ambao waliweza mtihani wa upimaji shuleni na kutambulika kama watahiniwa kutoka shule ya msingi Green Harvest.

“Tumekuwa na changamoto ya baadhi ya wazazi na walezi kutokulipa ada kwa wakati yanayosababisha mtoto kukosa haki yake ya msingi ya kusoma na huathiri maendeleo ya shule na kurudisha nyuma mikakati mingi ya shule,”amesema.

Kwa upande wake, Meneja wa shule hiyo, ambaye pia ni mmiliki, Bakari Kambi amewataka Watanzania kupeleka watoto wao katika shule hiyo ili waweze kupata elimu sahihi kwa maisha yao na kwa manufaa ya baadae.

Naye, Meneja Kitengo cha Uthibiti wa Viwango kutoka  Benk ya Equit Tawi la Dodoma, Dayandi Diyamett ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amesema kwa mujibu wa ripoti ya ufanisi wa sekta ya elimu ya mwaka 2018-2019 inaeleza takribani asilimia 43 tu ya watoto waliokuwa mashuleni ndio walioweza kumudu kubakia mashuleni mpaka kufikia kuhitimu kidato cha cha nne.

Dayandi ambaye  alimwakilisha Meneja wa Benk hiyo, Upendo Makula amesema asilimia 6.3 pekee ndio walioweza kujiunga na masomo ya chuo kikuu ambapo amedai vijana wachache wanaohitimu wakiwa na ujuzi wa kujiunga katika fani mbalimbali.

“Zipo sababu mbalimbali zinazofanya watoto kutokufikia ndoto zao za kutokuhitimu katika katika ngazi mbalimbali ikiwemo kukwama kwa wazazi kiuchumi,miundombinu mibovu ya kujifunzia,mimba na ajira za utotoni,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles