31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

‘Watanzania jengeni tabia yakuandika wosia’

Na Derick Milton, Simiyu

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) imewataka Watanzania kujenga tabia ya kuandika wosia, kwani kufanya hivyo itasaidia kwa kiwango kikubwa kuepusha migogoro ya mara kwa mara kwenye familia na kuwawezesha warithi halali kupata haki yao kwa wakati.

Akizungumza na hivi karibuni katika Kampeini ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) inayoendelea mkoani Simiyu, Afisa Sheria kutoka RITA, Grace Shao ameitaka jamii kuacha woga kuandika Wosia, kwani kufanya hivyo siyo uchuro na kusema baadhi ya watu wameandika na wanaendelea kuishi vizuri huku waliondika na wakafariki familia zao zimeendelea kuishi bila ya migogoro.

“Familia nyingi zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara juu ya mirathi, wengine wamedhulumiwa na ndugu ambao kisheria siyo waridhi wa mali, tumeendelea kuwaelimisha wananchi kuwa mwarobaini wa haya ni Wosia,” amesema Grace.

Aidha, Grace amewasihi wananchi kutumia taasisi ya RITA Katika kuandaa wosia kutokana na kuwa chombo cha serikali, lakini pia ni taasisi ambayo haina ukomo wa maisha pamoja na kuwa na wanasheria wabobevu wa masuala ya wosia na mirathi.

Katika hatua nyingine Grace amewahimiza wazazi kujenga tabia ya kuwatafutia vyeti vya kuzaliwa watoto ili kuondoa usumbufu wanaoweza kupata pindi watakapotakiwa kwenda kuanza shule na kuhitaji cheti cha kuzaliwa.

Amesema kuwa kwa sasa mtoto akitakiwa kwenda kuandikishwa shule lazima awe na cheti za kuzaliwa, kupata cheti cha kuzaliwa ni muhimu pia lakini pia ili mtu apate Bima ya Afya lazima cheti za kuzaliwa awe nacho.

“Tunawasihi wananchi mtoto akizaliwa ndani ya siku 90 ni muhimu kumtafutia cheti cha kuzaliwa, hii itasaidia kumtengenezea mtoto msingi mzuri wa majina yake pamoja na kumbukumbu yake ya tarehe za kuzaliwa.

“Kuna changamoto kubwa ya watu majina yao kuwa na shida, utakuta jina la shule ni tofauti na jina kuzaliwa, ikiwa hivyo huyo mtoto atapata shida wakati wa kutafuta kazi, lakini cheti cha kuzaliwa kinapotafutwa mapema inasaidia mtu kuwa na mtililiko mzuri wa majina yake,” amesema Grace.

RITA inaendelea Kutoa Huduma ya Usajili na kutoa Vyeti vya vya kuzaliwa, Elimu ya Mirathi,Kuandika na Kuhifadhi Wosia kwenye Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayoendelea kwenye viwanja vya Stendi ya zamani Mkoani Simiyu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles