Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM |
SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kuwataka wanafunzi wa elimu ya juu nchini kutofanya siasa vyuoni, wachambuzi na wanasiasa wamechambua agizo hilo huku wengine wakitofautiana.
Juzi, Rais Magufuli akiwa kwenye ziara katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro, aliwataka wanafunzi vyuoni kutojihusisha na siasa bali wasome na kufanya utafiti.
PROFESA BAREGU
Mchambuzi wa masuala ya siasa nchini, Profesa Mwesiga Baregu alisema vyuo ni mahali pa kutengeneza wanasiasa bora kwa sababu wanafunzi wa elimu ya juu si wa sekondari na shule za msingi.
“Rais amewakosea na kuwadharau wanavyuo kwa sababu ni watu wazima na ni wakati wao wa kuandaliwa na mustakabali wa taifa hili ni wao.
“Hivyo lazima waandaliwe waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwamo za jamii, siasa na uchumi.
“Nakumbuka wakati nafundisha wanafunzi walikuwa wakiuliza maswali yanayohusu siasa ili wawe raia bora hapo baadaye sasa kama wanazuiliwa kufanya siasa nadhani ni jambo lisilowezekana,”alisema Profesa Baregu.
PROFESA MPANGALA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha mkoani Iringa, Profesa Gaundence Mpangala alisema vyuo vikuu kwa kawaida wanachukuliwa kama watu wazima ndiyo maana sheria zao haziko kama sekondari na wanaweza kuoana na wakaendelea na masomo.
“Hivyo watu wazima si vizuri wasijihusishe na siasa kwa sababu …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.