23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MWENDOKASI KUHAMISHIWA KITUO MABASI UBUNGO


Na PATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM   |

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (Udart), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo(UBT).

Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika magari hayo.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika.

Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo waweze kufikia mwafaka.

“Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Meya alisema jambo hilo linaweza kupunguza mafuriko katika eneo la Jangwani na maeneo karibu na mto huo.

Alisema fedha za upanuzi huo zimekwisha kutolewa, kilichobaki ni utekelezaji wa mradi kuanzia daraja la Salendar hadi Pugu.

“Awamu ya kwanza ya mradi itaanzia Salendar hadi Kigogo, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo la mafuriko kwa wakazi wa Jangwani na maeneo jirani ya mto Msimbazi,” alisema.

DENI MACHINGA COMPLEX

Akizungumzia jengo la Machinga Complex, Meya Mwita alisema Halmashauri ya Jiji inadaiwa Sh bilioni 57 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles