LONDON, UINGEREZA
BAADA ya mchakato kwa kuchukua fomu kumpata mrithi wa Waziri Mkuu anayeondoka madarakani nchini Uingereza, Theresa May kufungwa, wagombea wa nafasi hiyo wameanza kujinadi huku wakionekana kutofautiana kuhusu muda wa nchi hiyo kujindoa Umoja wa Ulaya (EU).
Jumla ya wagombea 11 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo na kati yao anayepewa nafasi kubwa ya kushinda ni Waziri wa Mambo ya Nje, Boris Johnson
Kiongozi wa zamani wa Bunge la Uingereza Andrea Leadsom ambaye naye anawania nafasi hiyo amesema kujiondoa EU ifikapo mwishoni mwa mwezi Oktoba ni jambo gumu mno lakini linaweza kufanyika katika hali yeyote.
Hata hivyo mpinzani wake, Mark Harper alisema haiwezekani kuondoka ifikapo Oktoba 31, wakati Matt Hancock yeye amesema Brexit haiwezi kutatuliwa wa kutishia mpango wowote.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani, Sajid Javid, ambaye naye anawania nafasi hiyo alielezea kuwa ingawa alitaka kupitiwa upya kwa mpango huo, lakini iwapo watafika hadi mwishoni mwa Oktoba na chaguo likawa hakuna mpango au hakuna Brexit yeye atachugua hakuna mpango.
Tarehe ya mwisho ya Brexit ilipunguzwa nyuma ya Oktoba baada ya wabunge kukataa makubaliano ya May na Brussels kujiondoa mara tatu.
Umoja wa Ulaya umesema mara kwa mara kwamba makubaliano hayatafunguliwa tena, na mjumbe mkuu wa mazungumzo Michel Barnier anasisitiza kuwa “waziri mkuu mpya hatatabadili tatizo
BBC