Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
Kamishina Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi kwa kuwateua wakuu wa magereza wapya katika mikoa 19 Tanzania Bara (RPOs) na saba kuwabakiza katika nyadhifa zao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Deodatus Kazinja, Kasike ameteua maofisa sita kuwa wakuu wa vyuo vya magereza na kuwabadilisha maofisa watatu ndani ya jeshi hilo.
Katika mabadiliko hayo, kwa mara ya kwanza, amewateua wakuu wa magereza wa mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa magereza katika ngazi ya mikoa hiyo.
“Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (Dar es Salaam) SACP Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP Julius Ntambala, SACP Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake.
“Aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya) na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA.
“Aliyekuwa RPO (Mtwara) SACP Ismail Mlawa amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Mipango na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Varisanga Msuya aliyekuwa Kaimu Bohari Mkuu wa Jeshi na nafasi yake inachukuliwa na ACP Robert Masali ambaye anakuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza.
“Aliyekuwa RPO (Mwanza) SACP Athuman Kitiku amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya utumishi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP Hamza Hamza aliyekuwa RPO Tabora.
“ACP. Joseph Mkude anakuwa RPO (Tabora) na aliyekuwa RPO (Kagera) SACP. Boyd Mwambingu amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Utawala na nafasi yake inachukuliwa na ACP Rymond Mwampashe.
“Aliyekuwa RPO (Lindi) SACP Rajabu Bakari amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Mawasiliano na Usafirishaji na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Josephine Semwenda.
“Aliyekuwa RPO (Rukwa) SACP Benno Hunja amehamishiwa Makao Makuu sehemu ya Kilimo, Mifugo na Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na ACP Jail Mwamgunda na aliyekuwa RPO (Kilimanjaro) SACP Hassan Mkwiche amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Rajab Igongi. Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe ACP. Wilson Rugamba anakuwa RPO (Shinyanga).
“Waliokuwa Kaimu RPOs, vyuo na maeneo mengine ambao sasa wamethibitishwa ni kama ifuatavyo:- ACP. Hasseid Mkwanda (Iringa), ACP. Anderson Kamtearo (Arusha), ACP. Emmanuel Lwinga (Tanga), ACP. Masudi Kimolo (Manyara), ACP. Joel Matani (Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji), ACP. Rehema Ezekiel (Pwani), ACP. Msepwa Omary (Singida), na SP. Ally Uwesu (Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza).
“Walioteuliwa kuwa RPOs katika mikoa mipya ni ACP. Alexander Mmassy (Katavi), ACP. Lyzecky Mwaseba (Songwe), ACP. Festo Ng’umbi (Njombe), ACP. Robert Rumanyika (Geita) na ACP. Andulile Mwasampeta (Simiyu). Wakati huo huo ACP. Alexander Nyefwe anakuwa RPO (Ruvuma) na ACP. Leonard Burushi anakuwa RPO (Kigoma) kufuatia waliokuwa RPO katika mikoa hiyo kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
“Kwa mujibu wa Kamishna Jenerali Kasike, maofisa wote waliohamishiwa makao makuu wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Dodoma,” ilieleza taarifa hiyo