23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nondo alitaka Jeshi la Polisi lisake watekaji wake

Na ASHA BANI-DAR ES SALAM

SIKU chache baada ya kushinda kesi ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo na kudanganya kuwa alitekwa, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amejitokeza hadharani na kulitaka Jeshi la Polisi liwasake waliomteka.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Nondo alisisitiza kuwa alitekwa, lakini anamshukuru Mungu na atarudi chuoni kumalizia ngwe ya mwisho ya masomo yake.

“Kama mahakama imeniachia huru, inamaana watekaji wangu wapo, naamini Jeshi la Polisi litaendelea na kazi ya kuwasaka watesi hao ili wapatikane.

“Nawashukuru watetezi walionisimamia hadi leo na naahidi kurudi chuo kuendelea tena na masomo yangu kama hapo awali,” alisema Nondo.

Awali Kaimu Mratibu wa TSNP, Deogratius Bwire aliwataka polisi kuanza kuwatafuta watu waliohusika na utekaji kutokana na ukweli kwamba mahakama imeweka wazi kwamba upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha tuhuma kwamba Nondo alitoa taarifa za uongo kuhusu kutekwa kwake.

Aidha, Bwire pia amezitaka kanuni na sheria ndogo za vyuo zinazoruhusu kusimamishwa kwa wanafunzi wenye kesi mahakamani zifanyiwe marekebisho kwani zinakiuka haki za msingi za kikatiba.

Nondo aliachiwa Novemba 5, mwaka huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Liad Chemshana, ambaye alitoa hukumu katika kesi ya jinai namba 13 ya mwaka 2018.

Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Machi mwaka huu akikabiliwa na mashtaka mawili ya kutoa taarifa ya uongo kwa Ofisa wa Polisi wa Kituo cha Polisi Mafinga akidai alitekwa na watu wasiojulikana na kutoa taarifa za uongo mtandaoni aliyodaiwa kuyatenda Machi 7, 2018 akiwa Ubungo, Dar es Salaam.

Hakimu Chemshana alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mshatakiwa pamoja na Jamhuri hauna mashaka kuwa Nondo alikwenda polisi kama mlalamikaji ila polisi walimchukua kama mtuhumiwa .

“Mahakama hii imepitia ushahidi na majumuisho ya kesi hii   na kujiridhisha bila shaka yoyote kuwa makosa mawili ni  kueleza uongo na kurusha uongo mitandaoni, ni jambo  lisilo na ubishani, ila ni nani aliyeeleza taarifa hizo na kurusha uongo.

“Swali la kujiuliza je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga? Pili mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga, tatu hakuna ushahidi  toka Jamhuri kuwa mshtakiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa Jamhuri wametoa ushahidi wa hisia,” alisema na kuhoji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles