20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wakuu wa magereza   mikoani wapanguliwa

 Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

Kamishina Jenerali wa Magereza, Phaustine  Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi kwa kuwateua wakuu wa magereza wapya katika  mikoa 19  Tanzania Bara (RPOs)   na saba  kuwabakiza katika nyadhifa zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Deodatus Kazinja,   Kasike ameteua maofisa sita kuwa wakuu wa vyuo vya magereza na kuwabadilisha maofisa watatu ndani ya jeshi hilo.

Katika mabadiliko hayo, kwa mara ya kwanza, amewateua wakuu wa  magereza wa mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa  magereza katika ngazi ya mikoa hiyo.

“Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (Dar es Salaam) SACP Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP Julius Ntambala, SACP Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake.

“Aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya) na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA.

“Aliyekuwa RPO (Mtwara) SACP Ismail Mlawa amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Mipango na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Varisanga Msuya aliyekuwa Kaimu Bohari Mkuu wa Jeshi na  nafasi yake inachukuliwa na ACP Robert Masali ambaye anakuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza.

“Aliyekuwa RPO (Mwanza) SACP Athuman Kitiku amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya utumishi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP Hamza Hamza aliyekuwa RPO Tabora.

“ACP. Joseph Mkude anakuwa RPO (Tabora) na aliyekuwa  RPO (Kagera) SACP. Boyd Mwambingu amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Utawala na nafasi yake inachukuliwa na ACP Rymond Mwampashe.

“Aliyekuwa RPO (Lindi) SACP Rajabu Bakari  amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Mawasiliano na Usafirishaji na nafasi yake kuchukuliwa na ACP Josephine Semwenda.

“Aliyekuwa RPO (Rukwa) SACP Benno Hunja amehamishiwa Makao Makuu sehemu ya Kilimo, Mifugo na Mazingira na nafasi yake  inachukuliwa na ACP Jail Mwamgunda na aliyekuwa RPO (Kilimanjaro) SACP Hassan Mkwiche amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Rajab Igongi. Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe ACP. Wilson Rugamba anakuwa RPO (Shinyanga).

“Waliokuwa Kaimu RPOs, vyuo na maeneo mengine ambao sasa wamethibitishwa ni kama ifuatavyo:- ACP. Hasseid Mkwanda (Iringa), ACP. Anderson Kamtearo (Arusha),  ACP. Emmanuel Lwinga (Tanga), ACP. Masudi Kimolo (Manyara), ACP. Joel Matani (Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji), ACP. Rehema Ezekiel (Pwani), ACP. Msepwa Omary (Singida), na SP. Ally Uwesu (Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza).

“Walioteuliwa kuwa RPOs katika mikoa mipya ni ACP. Alexander Mmassy (Katavi), ACP. Lyzecky Mwaseba (Songwe), ACP. Festo Ng’umbi (Njombe), ACP. Robert Rumanyika (Geita) na ACP. Andulile Mwasampeta (Simiyu). Wakati huo huo ACP. Alexander Nyefwe anakuwa RPO (Ruvuma) na ACP. Leonard Burushi anakuwa RPO (Kigoma) kufuatia waliokuwa RPO katika mikoa hiyo kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

“Kwa mujibu wa Kamishna Jenerali Kasike, maofisa wote waliohamishiwa makao makuu wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Magereza  Dodoma,” ilieleza taarifa hiyo

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles